Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Jinsi ya Kuongeza uwezo wa RAM Kwenye Simu ya Android

Njia za kusaidia kuongeza RAM kwenye simu yako ya Android
Jinsi ya Kuongeza uwezo wa RAM Kwenye Simu ya Android Jinsi ya Kuongeza uwezo wa RAM Kwenye Simu ya Android

Kwa kawaida simu nyingi huja na kiasi cha kutosha cha RAM, lakini matumizi ya mtu binafsi ndio yanafanya simu kuwa na uwezo mdogo wa RAM. Sasa kuliona hili leo nimekuandalia njia rahisi ambazo unaweza kufuata ili kuongeza uwezo wa RAM ya simu yako.

Njia hizi ni rahisi na zinapatikana kwenye kila simu janja a.k.a Smartphone hivyo naimani kila mtu ataweza kufuatisha njia hizi moja kwa moja kwenye simu yake. Kumbuka kama simu yako imeanza kuwa slow na umejaribu kila namna na imeshindikana basi njia hii inaweza kusaidia simu yako kwa kiasi kikubwa sana.

Advertisement

Zima Wallpaper Zinazotembea Pamoja na Widget

Mara nyingi simu nyingi za Android zinakuja na Live Wallpaper Wallpaper hizi hutumia kiasi kikubwa sana cha RAM na kufanya simu yako kuishiwa na RAM kwa haraka.

Hii usababishwa na hatua ya wallpaper hizi kuwa kama video inayocheza kila wakati hata kama unatumia programu nyingine. Unacho takiwa kufanya ni kuweka wallpaper yenye rangi moja ya kawaida kwani itakusaidia sana kutunza chaji kwenye simu yako pamoja na RAM.

Jinsi ya Kuongeza uwezo wa RAM Kwenye Simu ya Android

Zima au Ondoa App Ambazo Huzitumii

Mara nyingi kume kuwa na tabia ya kuwa na app nyingi kwenye simu kiasi cha kufanya simu kuishiwa na RAM haraka kutokana na wingi wa app kwenye simu, hii huwa ni tatizo hasa pale apps hizo zinapo kuwa na mtindo wa kufunguliwa bila kufungwa.

Pendelea kuwa na tabia ya kuwa na apps ambazo ni muhimu kwako tu tena hasa kama uwezo wa RAM kwenye simu yako ni mdogo. Kama ni muhimu kuwa na app kama Facebook na Instagram basi download toleo la Instagram Lite au Facebook Lite. Pia unaweza ku- Force Close app kama huitumii kwa muda huo.

Jinsi ya Kuongeza uwezo wa RAM Kwenye Simu ya Android

Zima Animation Zisizo na Ulazima

Mara nyingi simu za Android huja na mbwembwe ambazo hizi huonekana pale mtu unapo fanya mambo mbalimbali, kwa mfano unapotoka kwenye sehemu moja ya app kwenda kwenye sehemu nyingine simu yako inaweza kuonyesha staili fulani ya jinsi kurasa zinavyofunguka. Sasa hii hutumia kiasi kikubwa sana cha RAM, hivyo ni muhimu sana kuweza kuzima sehemu hii.

Ili kuzima sehemu hii unatakiwa kuwasha sehemu ya Developer ambayo unaweza kuiwasha kwa kuingia kwenye Settings > About phone > Software Information > Kisha bofya mara 3 au mara 5 sehemu ya Build number, baada ya hapo utaona ujumbe kuwa sehemu ya Developer imewezeshwa. Sasa rudi kwenye Settings mwisho kabisa utaona sehemu hiyo ya Developer options.

Ingia kwenye sehemu hiyo kisha sehemu iliyo andikwa Window animation scale, bofya hapo kisha chagua 0.5X, baada ya hapo chini yake utaona Transition animation scale, nayo chagua 0.5x kisha chini yake utaona Animator duration scale, bofya hapo kisha chagua pia 0.5X.

Baada ya hapo toka kwenye ukurasa huo na utaona kuna mabadiliko ya mbwembwe hizo, pia unaweza kuzima kabisa sehemu hizo kwa kuchagua Animation Off kwenye kila hatua hapo juu.

Jinsi ya Kuongeza uwezo wa RAM Kwenye Simu ya Android

Angalia App Zinazotumia Kiasi Kikubwa cha RAM

Njia nyingine ya kuweza kutuza kiasi cha RAM kwenye simu yako ni kujua app zinazotumia kiasi kikubwa cha RAM, hii itakusaida kuchukua hatua za kuondoa app hizo au kutumia mbadala wa app hizo kama zipo.

Sasa kama unataka kujua app zinazotumia kiasi kikubwa cha RAM unaweza kufuata hatua hizi, Ingia kwenye Settings > Apps > Kisha chagua app yoyote kwa mfano Instagram kisha tafuta sehemu ya Memory kisha bofya hapo na utaona kiasi cha RAM app hiyo inayotumia.

Mara nyingi kama app inatumia zaidi ya MB 400 basi app hiyo inatumia RAM kiasi kikubwa.

Jinsi ya Kuongeza uwezo wa RAM Kwenye Simu ya Android

Na hizo ndio njia ambazo unaweza kuzitumia kuweza kuongeza kiasi cha RAM kwenye simu yako, kama kuna mahali bado hujaelewa unaweza kuuliza kupitia sehemu ya maoni hapo chini. Kujua maujanja zaidi ya Jinsi ya kuzuia simu kupata moto basi unaweza kusoma hapa. Kwa habari zaidi za teknolojia endelea kutembelea Tanzania Tech.

2 comments
  1. nimefuatilia hatua hizo nimekuta kwenye chrome ndiyo inakula ram ina 750 mb sasa ninafanyaje maana ni app ambayo imekuja na simu!,natumia tecno k7,asante.

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use