Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Subscriber YouTube Wamepungua ? Hizi Hapa Ndio Sababu

Kama umeona mabadiliko makubwa kwenye channel yako basi sababu ni hizi
YouTube Subscribers wamepungua YouTube Subscribers wamepungua

Kama wewe ni mmoja wa watu wenye channel kupitia mtandao wa YouTube basi inawezekana leo umeamka na kuangalia channel yako na kukutana subscriber wamepungua, kama ndio basi usipaniki sana kwani hatua hiyo ya kupunguza Subscriber imefanywa na YouTube.

Sasa kama ulikuwa hujui siku za karibuni YouTube ilitangaza kuwa inaenda kufanya zoezi la kupunguza akaunti feki kwenye mtandao wake, mmoja ya matokeo ambayo yangetokea kutokana na zoezi hilo kufanyika ni pamoja na kupungua kwa Subscriber kutoka kwenye Channel mbalimbali. Vilevile YouTube imeainisha kuwa channel zote ambazo pia zimepata subscriber kwa kununua kwa njia yoyote ile nje ya matangazo ya YouTube basi subscriber hao wataenda kuondolewa kwenye akaunti hiyo moja kwa moja.

Advertisement

Vilevile YouTube imedai kuwa, itaondoa channel zote ambazo hazitumiki au zilifungwa kwa namna moja ama nyingine, iwe channel imefungwa na mtumiaji mwenyewe au imefungwa kwa ajili ya kukiuka vigezo na masharti ya YouTube, channel zote za namna hiyo zitaondolewa.

Aidha YouTube imeandika kuwa, Channel zote ambazo zitaondolewa Subscriber na kushuka hadi kufikia subscriber chini ya 1000 basi channel hiyo haitaruhusiwa kuendelea kuonyesha matangazo kama sheria mpya za matangazo YouTube zinavyo sema.

Hivyo basi kama kwa namna yoyote ile umeona Channel yako imepungua Subscriber basi ujue hizo ndio sababu. Zoezi hilo limeanza kutekelezwa kuanzia tarehe 13 ya mwezi huu hadi siku ya jana tarehe 14, kutokana na kuwa tunapishana masaa basi channel nyingi za hapa Tanzania na Afrika mashariki kwa ujumla leo na kesho ndio zitaweza kuona mabadiliko ya Subscriber kwenye Channels nyingi. Kwa habari zaidi unaweza kusoma hapa.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use