Kama wewe ni mfutiliaji wa tovuti ya Tanzania tech basi ni wazi kuwa unajua jinsi ya kuondoa background kwenye picha bila kutumia app yoyote. Lakini tofauti na njia hii zipo njia nyingi ambazo ni bora zaidi ambazo zinaweza kusaidia kuondoa background kwenye picha kwa urahisi.
Moja ya njia hizo ni pamoja na njia hii ambayo nina kuonyesha leo ambayo na uhakika utaona ni njia bora kuliko njia ambayo tulionyesha hapo awali.
Kwa kuanza download app kupitia link hapo chini, kisha baada ya hapo install app hiyo kwenye simu yako. Baada ya hapo endelea kwenye maelekezo hapo chini.
Baada ya kuinstall na kufungua app bofya kwenye kitufe cha jumlisha kilichopo kuu katikati.
Baada ya hapo kama picha unayotaka kuondoa background ipo kwenye simu basi chagua Gallery, kama unataka kuondoa background kwenye picha unayoataka kupiga kwa sasa basi chagua sehemu ya kamera.
Baada ya kuchagua picha, moja kwa moja utaweza kuona mstari ukipita juu na chini, hiyo ikiwa ina ashiria picha hiyo inaondolewa background. Subiri kwa muda na moja kwa moja utaweza kuona picha ikiwa tayari imeondolewa background.
Baada ya hapo sasa unaweza kuchagua njia ya kusave picha yako na unaweza kutumia vitu hivyo vilivyopo upande wa kulia. Ukichagua kitufe cha box, utaweza kuchagua option kama Delete. Replace na Cutout.
Kitufe cha pili kitakusaidia kusave picha bila kuwa na sehemu nyeupe kama inavyo onekna hapo juu. Kwa kutumia sehemu ya Erase utaweza kufuta sehemu hiyo ya rangi nyeupe. Pia app hii itakupa uwezo wa kubadilisha vitu kama rangi ya picha na mengine mengi.
Kwa kufuata hatua hizo moja kwa moja utaweza kuondoa backround kwenye picha kwa urahisi na haraka. Kama unataka kujua njia nyingine zaidi unaweza kusoma njia iliyopita ya kuondoa background kwenye picha bila kutumia app yoyote.