Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Nunua Kamera (DSLR) Bora na Mambo ya Kuzingatia

Ukizingatia mambo haya utaweza kupata kamera bora kwaajili ya matumizi yako
Nunua Kamera (DSLR) Bora na Mambo ya Kuzingatia Nunua Kamera (DSLR) Bora na Mambo ya Kuzingatia

Kama wewe ni mmoja wa watu ambao wanafikiria kununua kamera ya DSLR basi kupitia makala hii nitaenda kukusaidia kununua kamera hiyo kwa kuonyesha mambo muhimu ambayo unatakiwa kujua kabla ya kununua kamera yako ya DSLR ya kwanza.

Njia hizi zime nisaidia mimi binafsi na nimeona leo nishiriki nanyi huku nikiwa na matumaini kuwa inaweza ku-kusaidia wewe kununua kamera bora.

Advertisement

Kupitia makala hii nitaenda kuonyesha mambo muhimu ambayo yatakusaidia kuweza kununua kamera bora ambayo itakufaa kwa matumizi yako ya kila siku iwe kwa matumizi ya kazi au binafsi. Basi bila kuendelea kupoteza muda twende moja kwa moja kwenye makala hii.

Matumizi ya Kamera

Kitu cha kwanza cha msingi ambacho unatakiwa kujua kabla ya kununua kamera ni kujua matumizi yako yako nini.?. Hii ni muhimu kwa kuwa itakusaidia sana kuchagua kamera bora. Zipo kamera ambazo ni bora kwa matumizi ya kupiga picha za mnato, na pia zipo kamera ambazo ni bora kwa kuchukua video, na pia zipo ambazo ni bora kwa picha mnato na video. Hivyo ni muhimu kujua matumizi yako kabla ya kuamua kununua kamera ya DSLR.

Kwa Matumizi ya Picha Mnato

Nunua Kamera (DSLR) Bora na Mambo ya Kuzingatia

Kama unataka kununua kamera bora kwa ajili ya picha basi ni muhimu kuangalia Mode ambazo zinapatikana kwenye kamera, unaweza kuangalia modes kama HDR Modes, Portrait Modes, Night Mode na nyingine. Pia hakikisha kamera inayo built-in flash na mengine.

Kwa Matumizi ya Video

Nunua Kamera (DSLR) Bora na Mambo ya Kuzingatia

Kama unataka kununua kamera kwa ajili ya video ni vyema kuangalia vitu kama resolution ya kamera, pia hakikisha una angalia frame rate. Kwa matumizi ya video ni vyema kununua kamera yenye uwezo wa frame rate hadi 60fps. Kadri frame rate inavyo kuwa juu zaidi ndivyo video inavyo kuwa bora zaidi.

Ukubwa wa Sensa (Sensor)

Ukubwa wa sensor ni moja kati ya kitu ambacho ni muhimu sana kuangalia kabla ya kununua kamera. Ni rahisi sana, kwani kadri sensor inayokuwa kubwa zaidi ndivyo ambayo kamera yako inakuwa na uwezo wa kuchukua picha na video zenye muonekano bora zaidi.

Kwa mujibu wa utafiti nilio fanikiwa kufanya zipo sensor za aina nyingi kwenye kamera, lakini zipo aina tatu za sensor ambazo ndio maarufu zaidi na zina patikana kwenye kamera nyingi za sasa. Aina hizo ni pamoja na Full frame, APS-C au (Advanced Photo System type-C) na Four Thirds.

Nunua Kamera (DSLR) Bora na Mambo ya Kuzingatia

Full frame Sensor

Full frame sensor ni sensor ambazo ni bora na zenye kuchukua video na picha angavu zaidi, kama jina la sensor hili linavyosema, kile unacho kiona kwenye kamera yako ndicho unacho kipata kwenye video au picha zako kwani picha au video hazina mkato au Crop Factor. Hata hivyo Full frame sensor ni bora zaidi kwa watu wanataka kununua kamera kwa ajili ya kupiga picha mnato.

APS-C (Advanced Photo System type-C)

APS-C sensor hii hupatikana zaidi kwenye kamera za bei nafuu na inakuja na uwezo wa kuchukua picha na video ambazo zina mkato au Crop Factor ya 1.6. Hata hivyo sensor hii ni bora zaidi kwaajili ya matumizi ya kupiga picha za mnato na hata video.

Four Thirds

Four Thirds hii hupatikana zaidi kwenye kamera zenye frame rate kubwa, na pia zinakuja na Crop Factor ya 2.0. Sensor hizi ni bora zaidi kwa matumizi ya kuchukua video zaidi kwenye kamera zenye sensor hizi kuwa na resolution kubwa zaidi.

Kifupi ni kwamba kama unataka kamera bora kwa ajili ya picha basi chagua kamera yenye sensor ya Full Frame, kama unataka kamera bora kwa video chagua Four Thirds na kama unataka kamera ambayo ni bora kwa video na picha mnato basi chagua APS-C Sensor.

Muundo wa Kamera

Japokuwa kamera nyingi za DSLR zinafanana kwa muundo lakini ni muhimu sana kuangalia muundo wa kamera kabla ya kununua, hii ni sambamba na kuangalia viunganishi vinavyo patikana kwenye kamera husika. Naposema viunganishi hapa namaana kama HDMI, na idadi ya ujumla ya viunganishi unavyopata kwenye kamera husika.

Nunua Kamera (DSLR) Bora na Mambo ya Kuzingatia

Pia ningependa kukushauri ununue kamera ambazo zinakuja na LCD Touch screen kwani hii itakusaidia sana hasa pale utakapo kuwa unataka kufanya vitu kwa haraka zaidi, pia kamera inayokuja na kioo au LCD ambayo inafunguka na kuzunguka ni bora zaidi hasa kama utakuwa umepanga kujirekodi au kujipiga picha wewe mwenyewe.

Nunua Kamera (DSLR) Bora na Mambo ya Kuzingatia

Lensi

Lensi ni kiungo muhimu sana pale inapokuja kwenye hatua ya kununua kamera, hivyo ni muhimu kuwa makini na brand unayotaka kununua kwani hii itakusaidia sana kupata lensi za aina mbalimbali hapo baadae utakapo hitaji.

Kwa mfano, Brand za Nikon, Canon pamoja na Sony ni brand ambazo ni maarufu zaidi hivyo ni rahisi kupata lensi za ziada pale utakapo hitaji. Hata hivyo, kwa mujibu wa utafiti niliofanya lensi za Nikon zinapatikana kwa bei nafuu zaidi kuliko lensi za Canon na Sony.

Hata hivyo unapo nunua kamera unaweza kupata lensi inayokuja na kamera yenye ya 18mm hadi 55mm. Hivyo kama upo kwenye bajeti na hutaki kununua kamera ya bei gali unaweza kununua kamera ya bei rahisi na baadae utaweza kununua lensi ya bei ghali na yenye uwezo mkubwa.

Nunua Kamera (DSLR) Bora na Mambo ya Kuzingatia

Megapixel

Kuangalia idadi ya megapixel kwenye kamera kabla ya kununua ni muhimu, lakini sio muhimu sana kama ambayo unadhani. Kamera inapokuwa na megapixel nyingi hii haina maana moja kwa moja kuwa kamera hiyo ina uwezo bora wa kupiga picha na kuchukua video.

Nunua Kamera (DSLR) Bora na Mambo ya Kuzingatia

Kifupi ni kuwa, kamera yoyote ambayo inatoka kwa sasa inakuja na megapixel za kutosha kwaajili ya matumizi yako ya kazi au binafsi. Hivyo basi usiangalie idadi ya megapixel kama kigezo cha mwisho cha kununua kamera ya DSLR.

Muda wa Kudumu

Mara nyingi inapokuja kwenye hatua ya ununuzi wa kamera ya DSLR ni muhimu kuangalia muda wa kudumu wa kamera. Hapa nina maana kuwa ni muhimu kununua kamera ambazo sio za miaka mingi sana iliyopita na ambazo zinaweza kuendelea kutumika kwa muda mrefu. Hii ni muhimu zaidi kama unataka kuwa na kamera yenye teknolojia ya kisasa.

Kama unataka kununua kamera ya kuanzia huku ukiwa na mawazo ya kununua kamera nyingine baadae pengine hatua hii inaweza isiwe ya muhimu kwako.

Kama upo kwenye bajeti na utanataka kununua kamera nzuri ya kupiga picha ni vyema kununua kamera ya Canon na Nikon ambayo inakuja na Sensor ya Full Frame sensor. Lakini kama unataka kununua kamera kwaajili ya video basi ni vyema kununua kamera yenye teknolojia ya 4K.

Nunua Kamera (DSLR) Bora na Mambo ya Kuzingatia

Hitimisho

Na hayo ndio mambo ya muhimu ambayo unahitaji kuangalia kabla ya kununua kamera ya DSLR, kama unalo jambo la kuongeza unaweza kutuambia kupitia sehemu ya maoni hapo chini. Unaweza pia kujifunza zaidi kuhusu Crop Factor kupitia hapa, pia kama unataka kujifunza mambo mengi zaidi hakikisha una subscribe kwenye channel yetu ya Tanzania Tech hapa.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use