Hapo siku ya jana, watumiaji wa mtandao wa Vodacom Tanzania walikumbwa na tatizo la kushindwa kutumia internet kwenye simu zako kwa siku nzima kutokana na tatizo la mtandao huo kushindwa kupata mawasiliano ya internet.
Kwa mujibu wa tovuti ya The Citizen, inasemekana kuwa Mkurugenzi wa Masuala ya Kampuni ya Vodacom, Rosalynn Mworia alisema kuwa huduma hiyo ilikuwa hapatikani siku ya jumapili kwa sababu ya kukatika kwa waya maalum wa mawasiliano ulipo chini ya maji huko Msumbiji ambapo marejesho yake yamekuwa ya muda mrefu kutokana na mvua nzito katika Bahari ya Hindi.
Hata hivyo kwa mujibu wa The Citizen, inasemekana kuwa Vodacom Tanzania ilitafuta suluhisho la haraka kutoka kampuni ya Seacom ambayo inajulikana duniani kwa kuwa kampuni ya kwanza Afrika kutengeneza mfumo wa kwanza wa internet ya waya inayopita katika pwani ya Afrika Kusini na mashariki.
Bi Mworia ambaye aliongea na The Citizen alisema kuwa, kampuni ya simu Vodacom Tanzania ilitafuta suluhisho la mpito kupitia mtoaji huduma wake wa msingi Seacom, ikiwa ni katika juhudi za kurejesha huduma ya mtandao. “Seacom itatupa uwezo mkubwa wa kurejesha huduma katika muda mfupi iwezekanavyo” alisema Bi Mworia.
Tunasikitika kwa usumbufu ulio jitokeza kwa wateja wetu, “alisema Bi Mworia zaidi ya hayo, kama kuthamini wateja wake kufuatia kukamilika kwa ukarabati huo kampuni hiyo imeahidi kutoa kiwango cha bando cha bure kwa watumiaji wake wote wa data mara tu huduma itakapokuwa imerejeshwa.
Hadi sasa huduma za internet za Vodacom Tanzania zinaonekana kurejea toka jana usiku, huku baadhi ya wateja wa mtandao huo wa simu wakiwa wamepewa fidia ya MB 300 kama kifuta machozi kutoka na kukosekana kwa hudma hiyo siku ya jana Jamapili, Februari 23, 2020.