Njia Bora ya Kudhibiti Matumizi ya Smartphone kwa Watoto

Kupitia njia hii utajua mwanao alipo, app gani anatumia zaidi na mambo mengine
Njia Bora ya Kudhibiti Matumizi ya Smartphone kwa Watoto Njia Bora ya Kudhibiti Matumizi ya Smartphone kwa Watoto

Katika ulimwengu huu wa sasa ni wazi kuwa ni muhimu sana kwa watoto walio na umri unaotakiwa kisheria kuwa na nyezo bora za kupata elimu ikiwa pamoja nyezo bora za mawasiliano kwaajili ya kuwasiliana na wazazi wote wawili.

Hii ni muhimu sana hasa pale watoto hao wanapo kuwa mazingira ya nyumbani.

Advertisement

Lakini wote tunakubaliana kuwa ni vigumu sana kwa siku hizi kuweza kujua kama watoto wetu wana tumia simu hizo kwa ajili ya mambo hayo na sio mambo ambayo ni kinyume na maadili.

Kuliona hili, leo Tanzania tech tunakuletea makala ambayo itaweza kusaidia wewe mzazi kudhibiti matumizi ya Smartphone kwa watoto wako na kuweza kujua kila kitu ambacho mwanao anafanya kwenye simu yake bila wewe kushika simu hiyo kila mara.

Kumbuka njia hii inafanyakazi kwenye vifaa vyote vya Android na iPhone venye sifa zifuatazo.

Kwa simu za Android

  • Kwa watumiaji wa simu za Android simu ya mwanao na yakwako inatakiwa kuwa na mfumo wa Android kuanzia Android 5.0 na kuendelea, pia mwanao anatakiwa kuwa na akaunti ya Google.

Kwa simu za iPhone

  • Kwa watumiaji wa simu za iPhone au simu zenye mfumo wa iOS simu hizo zinatakuwa kuwa na mfumo wa iOS kuanzia iOS 13 na kuendelea. Pia mtumiaji anatakiwa kuwa na akaunti ya Google. (Kumbuka kwa watumiaji wa iOS uwezo wa kuzuia vitu mbalimbali sio sawa na uwezo wa Android).

Baada ya kuhakikisha simu yako na ya mwanao inayo sifa zifuatazo basi moja kwa moja unaweza kuendelea kwenye maelezo hayo hapo chini.

Kwa kuanza hakikisha simu yako inayo Internet kwani kupitia hatua zote unatakiwa kufanya pale simu yako na ya mwanao inapokuwa imeunganishwa na Internet. Kama simu yako inayo Internet basi unaweza kuendelea kwenye hatua ya kwanza.

Hatua ya kwanza, wewe kama mzazi ingia kwenye soko la Play Store au App Store kisha download app ya Google Family Link for parent, unaweza kupakua app hiyo kupitia link hapo chini.

Google Family Link
Price: Free

Download Hapa Android

‎Google Family Link

Download Hapa iOS

Baada ya kudownload na kuinstall app hii kwenye simu yako basi moja kwa moja fungua app hiyo na itakupa maelekezo jinsi ya kuwezesha. Kitu cha muhumu hakikisha unayo akaunti ya google ya mwanao, kama mwanao hana akaunti basi  moja kwa moja unaweza kutengeneza ndani ya app hiyo bila kutoka nje.

Kama tayari mwanao anayo akaunti au kama tayari umesha unganisha akaunti yake kupitia app ya Google Family Link for parent, moja kwa moja sasa endelea kwa kuchukua simu ya mwanao na moja kwa moja ingia kwenye soko la Play Store na download app ya Google Family Link for child.

Download Hapa Android

Baada ya kuinstall app hii kwenye simu ya mwanao sasa ingiza Code ambazo umepewa kutoka kwenye simu yako wakati unafanya setup. Baada ya kuweka code hizo kwenye app hii kwenye simu ya mwanao moja kwa moja utaletewa sehemu mbalimbali ambazo utaweza kuanza kusetup.

Hatua zilizobaki ni rahisi na kwa sababu ya kuhakikisha kuwa watoto hawajui jinsi ya kuondoa app hii kwenye simu zao basi nitaishia hapa.

Kama wewe ni mzazi nakushauri kuuliza kupitia sehemu ya wasiliana nasi kama kuna mahali ambapo umekwama.

Uwezo wa App Hii

Baada ya hapo natumaini utakuwa umeweza kujua kila kitu mwanao anachofanya kwani app hii itaweza kukupa uwezo wa kuona data zake za WhatsApp na app nyingine, pia utaweza kuona mwanao alipo, pia utaweza kuona muda anaotumia kwenye app moja na nyingine na utaweza kumzuia kutumia app fulani hata kama uko mbali.

Utaweza kuzuia baadhi ya video kupitia mtandao wa YouTube ikiwa pamoja na sehemu ya comment. Pia utaweza kuzuia kutumia app fulani ndani ya muda fulani, pamoja na mambo mengine mengi sana jaribu app hii kisha njoo toa maoni hapo chini.

Usijalishe maoni yaliyopo kwenye soko la play store kwenye app ya watoto au Google Family Link for child. Hiyo ni kwasababu watoto hawaipendi kabisa kwa kuwa inafanyakazi inavyotakiwa.

Kujua zaidi unaweza kusoma hapa kujua app nzuri kwaajili ya katuni za watoto, unaweza kutumia app hii bila Internet hivyo nakushauri ujaribu app hii.

1 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use