Hivi karibuni kampuni ya Google ilitangaza kuja na programu yake mpya ya Google Reply programu hiyo ambayo ni maalum kwaajili ya watumiaji wa simu za Android. Inakuja ikiwa inatumia mfumo wa AI au Artificial Intelligence kuweza kukusaidia kubuni majibu ya meseji zako bila wewe kuandika.
Jinsi programu hiyo inavyo fanya kazi ni kuwa, baada ya kupakua na kuinstall app hiyo itaongeza sehemu maalum ya Google Reply kwenye programu zako za kuchati za Google Allo, Whatsapp, Facebook Messenger, Android Messages, Skype, Twitter DMs, pamoja na Slack, sehemu hiyo itakuwa inakuletea mapendekezo ya majibu ya meseji mbalimbali utakazo tumiwa kabla wewe kuandika majibu ya meseji uliyotumiwa.
Baada ya kuchunguza proramu ya majaribio nimegundua kuwa programu hiyo inafanya kazi vizuri iwapo unatumia lugha ya kingereza na sio lugha nyingine, mbali na hapo programu hiyo inafanya kazi vizuri sana na inarahisisha pale unapokuwa unachat na mtu kwa lugha ya kingereza.
Unaweza kujaribu programu hii kwenye simu yako ya Android kwa kupakua programu hiyo kupitia HAPA, kumbuka kwa sasa programu hii inafanyiwa majaribio kwa watu wa chache na bado haipatikani kwenye soko la Play Store hivyo ni muhimu kupakua programu hiyo hapo juu kwa sasa.