Miaka miwili iliyopita, Google ilitangaza ujio wa sehemu mpya ya Instant App, sehemu hii inakusaidia kuweza kujaribu App yoyote kupitia Play Store bila kuinstall kwenye simu yako. Yaani kuliko kuinstall app fulani na baadae ku-uninstall utaweza kujaribu App hiyo bila kuinstall kwenye simu yako.
Sasa sehemu hii ilikuwa bado haijafika kwenye Game bali ilikuwa ni kwenye programu za kawaida za Android, lakini hivi leo Google imetangaza ujio wa sehemu hiyo ya Google Play Instant ambapo sasa utaweza kujaribu Game mbalimbali kupitia Play Store bila ku-install kwenye simu yako ya Android.
Kwa sasa tayari zipo Game kadhaa ambazo unaweza kujaribu bila kuinstall. Unacho takiwa kufanya ni kuingia Google Play kwa kubofya link HAPA kisha chagua Game unayotaka kujaribu kati ya hizo na utaweza kuona kitufe cha TRY NOW bofya hapo kuweza kujaribu Game hiyo bila kuinstall kwenye simu yako.
Kwa sasa Game zenye uwezo wa kujaribu bila kuinstall ni chache, lakini Google imesema bado inaendelea kufanya maboresho ya sehemu hiyo na kuwataka watengenezaji wa Game kuwezesha sehemu hiyo wakati wana tengeneza Game hizo kwaajili ya simu za Android.