Kama wewe ni mmoja wa watu ambao walikuwa watafuta sana njia ya kuweza kuinstall Windows kwenye kompyuta yako kwa kutumia Flash basi njia hii ni kwa ajili yako.
Najua kuwa lazima unayo kompyuta ndio maana unasoma makala hii hivyo basi moja kwa moja ngoja niende kwenye mahitaji mengine ya muhimu. Kumbuka kwa kutumia njia hii unaweza kuinstall Windows 7, 8 pamoja na Windows 10. Pia kupitia makala hii nitaeleza zaidi kuhusu hatua za kutengeneza bootable USB Flash kwa hatua za ku-install windows tayari tulisha ziongelea.
TABLE OF CONTENTS
Mahitaji
Ili kuweza kuinstall Windows kwa kutumia USB Flash basi ni muhimu kabisa kuwa na USB Flash au USB Stick ambayo ina nafasi angalau GB 8 au zaidi, hii ni muhimu kwa sababu kadri muda unavyokwenda Windows inakuja na vitu vingi zaidi hivyo kuna wakatik GB 8 lazima zitakuwa hazitoshi kabisa.
Kama tayari unayo USB Flash basi hakikisha unakuwa na kompyuta ambayo inawaka, kwani hii ndio itakusaidia kuweza kutengeneza Flash hiyo ambayo utaweza kutumia ku install Windows. Pia vilevile unahitajika kuwa na file la Windows ambayo unataka, hakikisha file hilo linakuwa kwenye format ya .ISO.
Jinsi ya Kutengeneza Bootable USB Flash
Baada ya hapo basi sasa unaweza kuendelea kwenye hatua zifuatazo. Tembelea link hapo chini na hakikisha una download programu ya Windows USB/DVD Download Tool, baada ya kudownload install programu hiyo na kisha fungua.
Baada ya kudownload moja kwa moja fungua programu hiyo na sasa chomeka USB Flash yako kwenye kompyuta yako. Hakikisha Flash yako haina kitu na unaweza ku-format Flash yako kwa ajili ya kuhakikisha Flash yako haina tatizo lolote.
Baada ya hapo kwenye programu ya Windows USB/DVD Download Tool, chagua mahali ambapo ume hifadhi mfumo wa Windows kwenye kompyuta yako. (Hakikisha mfumo huo upo kwenye mfumo wa .ISO), Baada ya hapo bofya Next.
Kwenye ukurasa unao fuatia hakikisha unachagua sehemu ya USB Device ambayo itatokea upande wa kulia chini kama inavyo onekana kwenye picha hapo chini.
Hatua inayo fuata sasa hakikisha una chagua USB Flash yako kwenye list, hakikisha umefuata hatua zote za kuformat flash yako kwani bila kufanya hivyo inaweza isionekane kwenye hatua hii.
Baada ya hapo bofya sehemu ya Begin copying, baada ya hapo moja kwa moja utaweza kuona programu ya Windows USB/DVD Download Tool ikitengeneza bootable USB Flash. Sehemu hii huchukua muda kati ya dakika 20 au 25 kulingana na uwezo wa kompyuta yako. Subiri hadi programu imalize kabisa.
Baada ya hapo utaletewa ujumbe wa “Bootable USB Device created successfully“ na hapo utakuwa huko tayari kuinstall Windows kwa kutumia USB Flash yako.
Jinsi ya Ku-install Windows kwa Kutumia USB Flash
Sasa ili kuweza kuinstall mfumo wa Windows kwa kutumia USB Flash hiyo moja kwa moja zima kompyuta yako unayotaka kuinstall mfumo huo, kisha chomeka USB Flash hiyo kwenye kompyuta na moja kwa moja washa kompyuta yako.
Baada ya hapo bofya sehemu ya boot, sehemu hii huwa tofauti kwenye kila kompyuta na baada ya kubofya sehemu hiyo basi chagua jina la Flash yako ambalo litatokea kwenye kompyuta yako. Itakuwa na muonekano kama huo hapo chini.
Baada ya hapo sasa endelea kwenye hatua kwa hatua za kuinstall Windows ambazo zinapatikana kwa kusoma makala yetu iliyopita hapa.
Baada ya hapo utakuwa umemaliza hatua zate za kuinstall Windows kwenye kompyuta kwa kutumia USB Flash, ikiwa pamoja na hatua za kutengeneza Bootable USB Flash. Kama kwa namna yoyote hauna USB Flash unaweza kusoma makala yetu inayokuja ya jinsi ya kuinstall Windows kwenye kompyuta kwa kutumia simu yako ya Android.
Kama unataka kujifunza zaidi unaweza kusoma hapa kujua jinsi ambayo unaweza kuinstall Windows kwenye simu yako ya mkononi ya Android.