Kama wewe ni mtumiaji wa programu ya WhatsApp ni wazi kuwa usingependa kupoteza chats zako pale unapo badilisha simu ya mfumo mmoja kwenda mwingine, yaani kutoka Android kwenda iOS.
Kuliona hili leo nimekuandalia makala ambayo itaweza kuelekeza jinsi ya kuhamisha chat zako za WhatsApp zilizoko kwenye simu yako ya Android na kuziweka kwenye simu yako yenye mfumo wa iOS.
Njia hii ni rahisi lakini unahitaji kuwa na kompyuta kwani hii itaweza kurahisisha zaidi kazi nzima ikiwa pamoja na kufanya uweze kupata chats zako zote bila kupoteza chochote.
Basi bila kuendelea kupoteza muda moja kwa moja twende kwenye njia hizi ambazo na uhakika zitakusaidia kuamisha chat zako kwa urahisi kutoka Android kwenda iOS au iOS kwenda Android.
Kwa kuanza unatakiwa kupakua programu ya Dr Fone kupitia link hapo chini, baada ya hapo moja kwa moja install programu hiyo kwenye kompyuta yako kisha fungua programu hiyo, alafu fuata maelekezo haya.
Baada ya kufungua programu hii, kisha bofya sehemu ya WhatsApp Transfer iliyopo juu upande wa kulia.
Baada ya hapo, kama sehemu hiyo itahitaji download basi hakikisha una download sehemu hiyo kwani ina MB chache sana, kama hamna haja ya kudownload basi endelea kwa kwa kuchagua sehemu ya kubackup kwanza, hii ni muhimu kama kutatokea jambo lolote.
Baada ya hapo chomeka simu ambayo unataka kutoa WhatsApp meseji zako.
Baada ya kuchomeka simu yako moja kwa moja utaweza kuanza kuona chat zako za WhatsApp zikihifadhiwa kwenye kompyuta yako kwa kutumia programu hii.
Baada ya kukamilisha backup, moja kwa moja utaweza kuona ujumbe mfupi ambao unaonyesha kuwa backup imekamilika.
Baada ya hapo bofya OK kisha moja kwa moja chomoa simu yako ya Android au simu ambayo ulikuwa unataka kutoa chats zake kisha moja kwa moja chomeka simu yako ambayo ambayo unataka kuhamishia chats zako.
Baada ya kuchomeka simu yako kwenye kompyuta, moja kwa moja endelea kwa kubofya sehemu ya Restore WhatsApp Messages to iOS device. Hakikisha unafanya hivyo simu yako ya iOS ikiwa imechomekwa kwenye kompyuta.
Baada ya hapo, endelea kwa kuchagua backup unayotaka kurestore, kisha moja kwa moja bofya Next kwenye sehemu ya chini ya programu hii.
Baada ya hapo, kama hujachomeka simu yako vizuri hatua hii itakuta uhakikishe umefanya hivyo, kama umechomeka simu yako vizuri basi moja kwa moja bofya sehemu ya Restore.
Kama kwenye simu yako ya iOS kunayo programu ya WhatsApp ambayo tayari umesha anza kutumia basi kwenye hatua hii bofya Yes, kama huna programu ya WhatsApp ambayo unatumiwa kwa sasa moja kwa moja bofya No.
Kupitia mfano huu ninayo programu ya WhatsApp lakini situmii programu hivyo nitabofya No, baada ya hapo moja kwa moja endelea kwa kubofya Restore.
Baada ya hapo, unatakiwa kuingia kwenye programu ya WhatsApp kwenye simu yako ya iOS, hakikisha unafanya hivyo simu yako ikiwa imechomekwa kwenye kompyuta. Kama huna programu ya WhatsApp kwenye simu hiyo hakikisha una download kwenye hatua hii kisha setup programu hiyo na kisha endelea kwenye hatua inayofuata.
Baada ya kukamilisha kuingia kwenye programu yako ya WhatsApp kwenye simu yako ya iOS basi moja kwa moja bofya sehemu ya Continue iliyotokea kwenye programu hii ya Dr. Fone.
Baada ya hapo utaweza kuanza kuona moja kwa moja meseji zako zilizokuwa kwenye simu ya Android, zikiamishwa kuingia kwenye simu yako ya iOS au simu unayotaka.
Sehemu hii huchukua muda kulingana na wingi wa meseji ulizonazo kwenye chat zako zilizokuwa kwenye simu yako ya Android.
Baada ya kumaliza simu yako ya iOS itajizima na kujiwasha na moja kwa moja utaweeza kuona chat zako zote zilizokuwa kwenye Android zimehamia kwenye simu yako yenye mfumo wa iOS.
Kwa kufuata hatua hizo moja kwa moja utaweza kuhakimisha chats zako kutoka kwenye simu yako ya Android kwenda kwenye simu yako ya iOS.
Kama unataka kujua zaidi unaweza kuondoa pattern kwenye simu yako ya Android kwa kutumia programu hii ya Dr.Fone hivyo unaweza kufanya mengi sana kwa kutumia programu hii, kama vile kurudisha mafile yaliyofutika kwenye simu yako na mambo mengine mengi.
Kama unataka kuendelea kujifunza zaidi hakikisha unatembelea tovuti ya Tanzania tech kila siku.