Mamlaka ya mawasiliano ya Tanzania kwa kushirikiana na kampuni za simu za Tanzania imeleta huduma mpya ya kuwawezesha wateja kuhama mtandao bila kubadilisha line. Kwa mujibu wa wakala wa huduma kwa wateja wa Vodacom ambae nilizungumza nae, huduma hiyo itanza kuanzia tarehe 1 mwezi March mwaka huu 2017 na itahusisha mitandao yote ya simu.
Kwa mujibu wa wakala huyo wa huduma kwa wateja mteja atapata uwezo wa kubadili line yake kwenda mtandao mwingine wowote pale anapo amua kuhama. Yani kwa mfano pale unapo ona kuwa huitaji kuwa kwenye mtandao wa Vodacom na unataka kuhamia Tigo basi hapo utaenda kwenye ofisi za mtandao wa tigo ukiwa na kitambulisho ulicho sajilia line yako hapo awali ukiwa kwenye mtandao wa Vodacom na baada ya hapo Tigo watabadilisha line yako hiyo kuwa ya mtandao wa Tigo.
Kumbuka kabla ya kufanya hivyo unatakiwa kutoa pesa zote kutoka kwenye huduma za simu bank pamoja na salio la muda wa maongezi kwenye line yako hiyo kabla hujamua kuhama mtandao, kwani kwa kubadili line yako kutafanya huduma zote za awali ulizokua nazo kwenye line yako kufungwa kabisa kwa kipindi chote ambacho utakua umeamia mtandao mwingine. Kuhusu code namba za mwanzo yani 071** au 075** hazita jalisha bali pale mteja wa mtandao ambao ulikua awali atakapo kupigia atapewa ujumbe kuwa line yako ni ya vodacom lakini kwa sasa umeamia mtandao mwingine. Kwenye huduma hii mpya mteja ataruhusiwa kurudi kwenye mtandao wake wa awali baada ya siku 30 yani mwezi mmoja na sio vinginevyo.
Huduma hii inatarajiwa kuanza rasmi kuanzia tarehe ya kwanza ya mwezi March hivyo kama bado ujapokea ujumbe kutoka kwenye mtandao wako basi habari ndio hiyo, kuanzia mwezi ujao utakuwa na uwezo wa kutumia line moja kwenye mitandao mingine kama utakua unataka kuhama mtandao. Kwa habari zaidi kuhusu hili tembelea wakala wa mtandao wako au piga simu huduma kwa wateja na ulizia kuhusu huduma hii mpya.
Kuwa wa kwanza kupata habari zote za teknolojia kwa kudownload App ya Tanzania Tech kupitia Play Store au kama unataka kupata habari na maujanja mbalimbali kwa njia ya video basi junge na channel yetu ya Tanzania Tech kupitia Youtube.
Nimeipenda sana hii taarifa alafu pia nimependa hii, blog mana nakumbuka ndio iliyokuwa ya kwanza kutangaza habari hii kbla ya blo yoyote ile hivyo napenda kwataarifu wana timu wote wa Tanzania Tech kuwa nategemea sana blog yenu kupata taarifa mpya na zenye uhakika. Asante sana Tanzani Tech keep it up.