Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Jinsi ya Kufuta kwa Haraka Majina Yaliyo Jirudia

Jifunze namna rahisi ya kufuta majina yaliyojirudia kwenye phonebook ya simu yako
Jinsi ya Kufuta kwa Haraka Majina Yaliyo Jirudia Jinsi ya Kufuta kwa Haraka Majina Yaliyo Jirudia

Kuna wakati unajikuta una hifadhi majina mara mbili kwenye phonebook ya simu yako, mara nyingi hii usababishwa na kuunganisha akaunti yako ya Google pamoja na Phonebook ya simu yako, pia vilevile wakati mwingine husababishwa na ku copy majina kutoka kwenye line yako kuja kwenye simu yako.

Kujirudia kwa majina wakati mwingine ni usumbufu mkubwa na pale unapo amua kufuta au kuondoa majina hayo yaliojirudia ukweli ni kwamba unaweza kujikuta umetumia muda mrefu sana.

Advertisement

Kukusaidai katika hilo leo Tanzania Tech tunakuletea njia mbalimbali na rahisi za jinsi ya kufuta majina yaliyojirudia kwenye phonebook ya simu yako ya Android.

Kwa Kutumia Phone Contacts

Simu nyingi za sasa zinakuja na sehemu maalum ambayo inakusaidia kuweza kufuta majina yaliyojirudia kwenye phonebook yako. Ili kuweza kufuta majina, fungua Contact kwenye simu yako kisha bofya Menu alafu bofya “Manage Contact” kisha bofya “Merge accounts” kisha chagua “Merge from Google” kisha malizia kwa kubofya OK.

Baada ya hapo utaona majina yote yaliyojirudia kutokana na kujiunga na akaunti ya google yakijiuondoa, kumbuka njia hii inaweza isiondoe majina yote yalio jirudia hivyo ni vyema kufuatilia hatua inayofuata.

Kwa Kutumia Akaunti ya Gmail

Kama unataka kutunza kumbukumbu ya majina yako ni lazima utakuwa umewasha sehemu maalumu ya “contact syncing” kwenye simu yako ya android, sehemu hii inakusaidia kuifadhi kumbukumbu ya majina yako ili kuweza kuyapata pale simu yako inapo haribika au kupotea.

Sehemu hii mara nyingi huwa ina kuwa imejiwasha yenyewe hivyo hata kama hujawahi kuiwasha basi uwezekano wa sehemu hiyo kuwa imewashwa ni mkubwa.

Kama sehemu hii imewashwa kwenye simu yako basi ni rahisi sana kufuta majina yaliyojirudia kwenye simu yako, ili kufanya hivyo tumia kompyuta yako kuingia kwenye email yako ya Gmail kisha bofya kitufe cha Gmail kilichopo upande wa kushoto juu kisha chagua Contact.

Jinsi ya Kufuta kwa Haraka Majina Yaliyo Jirudia

Baada ya hapo utaona majina yako yaliyoko kwenye simu yako. Baada ya hapo chagua sehemu iliyoandikwa Merge & Fix inayopatika upande wa kushoto. Kisha malizia kwa kubofya sehemu ya Merge Duplicate.

Kwa kifanya hivyo utaona majina yote yaliojirudia ili kuyafuta bofya kitufe kilicho andikwa merge.

Jinsi ya Kufuta kwa Haraka Majina Yaliyo Jirudia

Kama utafuata hatua zote hapo juu basi utakuwa umeweza kufuta majina yaliyojirudia kwenye simu yako ya android iliyounganishwa na email hiyo. Kama bado kuna majina yaliyojirudia basi tumia njia nyingine inayofuata.

Kwa Kutumia Programu Maalum

Kama utakua umejaribu njia zote hapo juu na bado unaona kuna majina yaliyojirudia basi unaweza kutumia programu hizi ambazo ni rahisi sana kutumia.

Contacts Optimizer

Contacts Optimizer
Price: Free

Download Hapa

Simpler Merge Duplicates

Easy Contacts Cleaner
Price: Free

Download Hapa

Kama umepata tatizo lolote kuhusu programu hizi unaweza kutuandikia kwenye maoni hapo chini nasi tutakulekeza namna ya kutumia programu hizi moja kwa moja.

Kwa kufuata hatua zote hizo basi lazima utakuwa umeweza kuondoa majina yote yaliyo jirudia kwenye phonebook ya simu yako ya Android.

Kama unataka kupata mafunzo kama haya kwa haraka unaweza kudownload App ya Tanzania Tech au unaweza kujiunga na channel yetu ya Tanzania Tech kupitia Mitandao wa Youtube na utapata habari mpya kila siku kwa haraka zaidi.

8 comments
  1. mimi simu yangu ya Samsung s9 haisevu majina ya simu kweny simu card ila inasevu kwenye email au phone tatizo ni nini mkuu

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use