Kama wewe ni mmoja wa watu ambao wamewahi kuwa waanga wa kufungiwa akaunti na instagram bila taarifa basi hii ni kwajili yako. Mtandao wa instagram hivi karibuni unategemea kufanya mabadiliko kwenye sehemu hiyo na kuanza kutoa taarifa kabla ya kufunga akaunti yoyote ya Instagram.
Kwa mujibu ripoti kutoka tovuti ya habari ya Instagram, hapo awali mtumiaji wa instagram ambaye amekiuka au kuvunja sheria za mtumizi ya mtandao huo akaunti yake ilikuwa ikifungwa au kufutwa moja kwa moja bila taarifa yoyote. Lakini hivi sasa instagram imefanya mabadiliko ya sehemu hiyo na endapo akaunti yako imekiuka vigezo na masharti ya utumiaji utapokea ujumbe wenye kufamisha kuwa umevunja sheria za matumizi ya mtandao huo na akaunti yako ipo hararini kufungwa.
Mbali ya kupewa taarifa hizo, pia utapewa sababu za kwanini akaunti yako iko mbioni kufungwa pamoja na hatua ambazo instagram imechukua. Vilevile instagram imebainisha kuwa, watumiaji ambao watakuwa wanapokea meseji hizo mara kwa mara ndani ya kipindi cha muda mfupi, akaunti zao zitafungiwa mara moja.
Facebook kwa sasa inapambana kuhakikisha mtandao wa Instagram unakuwa salama, siku za karibuni mtandao huo pia ulileta sehemu mpya inayotumia mfumo wa AI ili kutambua maoni au comment za matusi pale mtu atakapo kuwa anataka kutuma kwa mtu mwingine, sehemu hiyo itakuwa inakupa ujumbe ambao unakutaka uwe muangalifu na maoni au comment unazotaka kutuma.
Kwa sasa sehemu hizo zote ziko mbioni kufikia watumiaji wote wa mtandao wa Instagram, hivyo kama bado hujaona sehemu hizi fahamu ni kwa sababu sehemu hizi zinakuja kwa awamu. Kwa habari zaidi kuhusu hili endelea kutembelea Tanzania Tech kila siku, kama unataka kujifunza zaidi unaweza kusoma hapa kujua njia mpya za kutumia mtandao wa Instagram.