Ni wazi kuwa watu wengi sana bado wanatumia memory card kuhifadhi vitu mbalimbali vya muhimu, iwe unatumia memory card kwenye simu au hata kwenye kamera ya kidigitali ukweli unabaki pale pale kwamba, bado memory card ni sehemu muhimu ya vifaa vyetu vya kielektroniki.
Lakini tatizo linakuja, mara nyingi memory card hupoteza uwezo wake wa kufanya kazi bila hata sababu ya msingi, yaani inakuwa kama vile memory card hiyo imeisha muda wake wa kufanya kazi yani inakufa tu bila hata wewe kutegemea.
Sasa kama wewe ni mmoja wa watu ambao wamekutana na tatizo hili basi leo nimekuletea njia ambayo na uhakika ukitumia inaweza kusaidia kufufua memory card yako bila hata kupoteza chochote kilichopo ndani ya memory card hiyo.
Kitu cha msingi unachotakiwa kuzingatia ni kuwa na kompyuta ya Windows kwani hatua zote zinafanyika kupitia kompyuta. Basi kama unayo kompyuta yenye mfumo wa Windows basi endelea kwenye hatua zinazofuata.
Kwa kuanza chomeka memory card yako kwenye kompyuta, kisha baada ya hapo bofya kwenye sehemu ya kutafuta ya Windows kisha andika maneno CMD. Baada ya hapo Right Click kwenye sehemu ya Command prompt kisha chagua Run as administration.
Baada ya hapo programu ya command prompt itafunguka na endelea kwa kuandika maneno haya kwenye sehemu ya command, andika chkdsk / alafu andika herufi ya flash yako jinsi inavyo onekana kwenye computer yako kisha malizia kwa kuandika /f. Kwa mfano kama memory card yako inaonekana kwenye Windows ikiwa na herufi E basi itakuwa kama kwenye picha hapo chini.
Baada ya kumaliza bofya Enter kwenye keyboard ya kompyuta yako, utaona programu hiyo ikianza kuangalia memory card yako na moja kwa moja utaona memory card yako imefanikiwa kupona. Kumbuka kama njia hii haito fanya kazi basi tuandikie kupitia maoni hapo chini tutakujuza njia nyingine ya kuweza kusaidia.
Kama unataka kujua njia ya kufufua flash iliyokufa unaweza kusoma hapa ili kujua njia ambazo zinaweza kusaidia kufufua flash yako kwa kutumia kompyuta.
Kwa maujanja zaidi kama haya hakikisha una subscribe kwenye channel yetu kupitia mtandao wa YouTube kwani utaweza kujifunza maujanja haya yote kwa vitendo. Kwa habari zaidi za teknolojia hakikisha unaendelea kutembelea tovuti ya Tanzania Tech kila siku.
Maoni*nitawezaje kufufua memory card kwa kutumia sim janja.
Hapana, kwa sasa bado njia hiyo haijafanyiwa kazi.
Je nawezaje kufufua flash ambayo ukichomeka kwenye computer inaonesha kama ipo ila haionekan..
Iko poa
Hi!
Nimejaribu kufufua sd card yangu/memory card nimeshindwa,nimepata reply isemayo,”cannot open volume for direct access”. vp hapo mkuu,naomba maujanja hapa.
mbona nimejaribu lakini hamn kitu
Umefuata hatua zote kwa usahihi..?
Nawezaje kukufua memory card Kwa kutumia smartphone??
Asante kwa maoni.
wakikujibu ni tag
Memory card haisomi kwenye PC kuna njia nyingine je mana sijaweza kuona jina la memorycard
Vpkwa memory ambayo haisomi kwenye computer inakuwaje?
nimejalibu hii njia imegoma kufanya kazi,
nikichomeka memory kweny computer inaniomba kuformat nikiformat inafali
mbona memory card haionekani kwenye computer
Kivipi haioniekani, ilikuwa inaonekana kabla..?
nimejaribu hii njia ila inakataa inakataa inaandika formart
nimefuata hatua zote ila inanidai kuformat nikiformat inaniambia disk write protected
Nataka kufufua SD card kwa simu ya mkononi smart nifanyaje