Kama wewe ni mmoja wa watu wanaofuatiia taarifa mbalimbali mtandaoni basi lazima unajua kuwa kampuni ya Xiaomi tayari ipo Tanzania na tayari simu za Redmi Note 8, na Redmi 8 pamoja na Redmi 8A zipo sokoni nchini Tanzania.
Lakini kutokana na simu hizi kuanza kuwepo kwa hapa nchini Tanzania, nimeona kuna haja ya kujuzana jinsi ya kuflash simu hizi hasa kama utakuwa umekutana na matatizo mbalimbali kwenye simu yako. Kumbuka njia hii inaweza kukusaidia kuflash simu ya aina yoyote ya Xiaomi au Redmi kama zinavyo tambulika kwa sasa.
Pia ni muhimu kujua njia hii isitumike vibaya hasa kama unataka kuflash simu ambayo sio yako au kuflash simu ambayo sio ya kwako ni kinyume na sheria za Tanzania hivyo hakikisha huvunji sheria za nchi kwa namna yoyote. Mbali na hayo pia ni muhimu kuwa makini kwani unaweza kuharibu simu yako hivyo kuwa makini kwani hatuto husika pale utakapo haribu simu yako au kuvunja sheria kwa namna yoyote. Makala hii ni kwa ajili ya kujifunza tu.
Basi baada ya kusema hayo basi moja kwenye moja twende tukajifunze jinsi ambayo unaweza kuflash simu yako ya Xiaomi au Redmi kwa kutumia kompyuta.
TABLE OF CONTENTS
Mahitaji
Kabla ya kuanza kuflash simu yoyote au simu ya Xiaomi au Redmi ni lazima kuwa na mambo haya ya muhimu, jitahidi kuhakikisha unakuwa na kila kitu hapa kabla ya kuendelea.
- Waya wa USB unaokuja na simu au wenye uwezo wa kusoma data kwenye simu yako.
- Kompyuta yenye mfumo wa Windows kuanzia Windows 7, 8, na Windows 10.
- Unatakiwa kuwa na bando angalau GB 3, unaweza kusoma hapa ili kujua vifurushi vya bei rahisi ya ambavyo unaweza kujiunga kwa sasa.
- Unatakiwa kuwa na programu ya kuflashi ya Xiaomi inayoitwa Mi Flash Tool. Unaweza kupata programu hiyo kwa kupakua kupitia hapo chini.
Download Mi Flash Tool for Windows
Programu ya Mi Flash Tool inapatikana kwenye matoleo mbalimbali. Tume kuwekea link ya programu zote za Mi Flash Tool. Toleo jipya la programu hiyo linapatikana hapo chini huku matoleo ya zamani yakiwa yanapatikana chini kabisa.
Name | Xiaomi Mi Flash Tool |
Version | v20191206 |
Size | 82.3 MB |
Compatible | Windows 7/8/8.1/10 |
Old Mi Flash Versions (Download Links)
Mi Flash Tool v4.5.9 | Download |
Mi Flash Tool v5.6.1 | Download |
Mi Flash Tool v5.6.1 | Download |
Mi Flash Tool v5.10.28 | Download |
Mi Flash Tool v6.4.1 | Download |
Mi Flash Tool v6.8.30 | Download |
Mi Flash Tool v6.12.22 | Download |
Mi Flash Tool v7.4.25 | Download |
Mi Flash Tool v7.12.12 | Download |
Mi Flash Tool v8.5.28 | Download |
Mi Flash Tool v8.11.15 | Download |
- Kitu kingine unachotakiwa kuwa nacho ni mfumo wa uendeshaji wa simu unayotaka kuflash (Firmware) zipo tovuti mbalimbali mtandaoni zinazotoa huduma ya kupakua firmware lakini unaweza kujaribu tovuti ya xiaomifirmwareupdater.com.
Jinsi ya Kuflash Simu za Xiaomi (Redmi)
Baada ya kuwa na kila kitu kwenye list hiyo sasa upo tayari kuendelea kwenye hatua zinazofuata za kuflash simu za Redmi au Xiaomi. Hakikisha unafuata hatua kwa hatua.
Hakikisha una download firmware ya simu yako na pia una install programu ya Mi Flash tool kwenye kompyuta yako, baada ya hapo fungua programu hiyo na chini upande wa kulia utaona sehemu tatu, Flash All Except Data & Storage”, “Flash All Except Storage” na “Flash All.
Sehemu hizo ni muhimu sana kwani kwa kuchagua Clear all hii programu itafuta kila kitu kilichopo kwenye simu yako mara baada ya kuflash, na ukichagua save user data basi programu hii uhifadhi data zako za muhimu mara baada ya kuflash, kuchagua clear all and lock programu hii hufuta kila kitu lakini hufunga simu yako kama ilivyokuwa.
Baada ya hapo sasa bofya upande wa juu kushoto utaona sehemu imeandikwa “Select” bofya hapo kuchagua file la simu yako subiri kidogo kisha endelea kwa kubofya Flash iliyopo sehemu ya upande wa kulia juu. Baada ya hapo utakuwa umemaliza kuflash simu yako ya Android ya Xiaomi au Redmi.
Kama unataka kujifunza jinsi ya kuflash simu za TECNO unaweza kusoma hapa, pia kama unataka kujua jinsi ya kuflash simu za Samsung unaweza kusoma makala ya hatua kwa hatua hapa. Kwa maujanja zaidi hakikisha unaendelea kutembelea Tanzania Tech kila siku.
Unaflash vp bila ku unlock bootloader
Njia hii inafanyakazi kama simu yako iko unlocked bootloader.