Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Jinsi ya Kuflash Simu Mpya za Nokia Kwa Kutumia Kompyuta

Soma hapa hatua kwa hatua jinsi ya kuflash simu za mpya za Nokia
Jinsi ya Kuflash Simu Mpya za Nokia Kwa Kutumia Kompyuta Jinsi ya Kuflash Simu Mpya za Nokia Kwa Kutumia Kompyuta

Kama wewe ni mmoja wa watu wanaotumia simu mpya za Android ya Nokia, basi ni vizuri kujua kuwa sasa programu ya kuflash simu hizo mpya za Nokia inapatikana kwa watumiaji wa kawaida.

Awali programu hii ilikuwa haipatikani kwa watumiaji wa kawaida na ilikuwa ni maalum kwa wafanyakazi wa kampuni ya HMD Global kampuni ambayo ndio inaendesha na kusimamia upatikanaji wa bidhaa za Nokia.

Advertisement

Hata hivyo kwa sasa unaweza kudownload programu hiyo ambayo inakuja na hatua maalum ambazo ni muhimu kuzifuata ili kuweza kuflash simu yako kwa usahihi. Hatua hizo ni pamoja na kuhakikisha simu yako inapatikana kwenye list ya simu zenye uwezo wa kuflashiwa na programu hiyo, list ya simu zenye uwezo wa kuflashiwa na programu hii ni kama ifuatayo.

Kama simu yako iko kwenye list hiyo basi unaweza kuendelea kusoma makala hii ili kujua jinsi ya kuflash simu kwa kutumia programu hiyo pamoja na jinsi ya kuinstall programu hiyo.

Programu ya Kuflash Simu za Nokia

Kama nilivyo kwambia hapo juu, programu hii mpya inaitwa Nokia Online Service Tool (OST) na ili kuinstall kwenye kompyuta yako ya Windows unahitaji kuhakikisha kompyuta yako ina mfumo mpya wa Windows 10, Windows 7 au Windows 8.

Kama unavyo vyote hivyo sasa unaweza kupakua mfumo huu na kuinstall kwenye kompyuta yako, yako mafile mawili na yote yana umuhimu mkubwa hivyo hakikisha una download mafile yote.

Firmware za Simu Mpya za Nokia

Pia kama unataka kupakua mfumo mpya wa simu za Nokia unaweza kufanya hivyo kwa kutembelea tovuti mbili kati ya hizo ambazo tumekuwekea hapo chini.

Ku-install Nokia Online Service Tool (OST)

Kama tayari umesha download programu ya OST au Nokia Online Service Tool, na kama pia tayari unao mfumo wa Android wa simu yako sasa endelea kwenye hatua za jinsi ya kuinstall programu hiyo. Hatua hizi ni za muhimu sana na ni vyema kufuata hatua kwa hatua mpaka mwisho.

  • Fungua programu ya Nokia Online Service Tool (OST) ambayo iko kwenye file la ZIP na fungua ndani yake kisha bofya mara mbili file lilo andikwa ‘launcher.exe’.

Jinsi ya Kuflash Simu Mpya za Nokia Kwa Kutumia Kompyuta

  • Baada ya hapo endelea kwa kubofya Next na pale programu hii inapo maliza ku-install maliza kwa kubofya Close.

Jinsi ya Kuflash Simu Mpya za Nokia Kwa Kutumia Kompyuta

  • Hatua inayofuata ni ya MUHIMU sana na hii ndio itafanya programu hii kuweza kufanya kazi kwa usahihi. Sasa fungua file la Nokia OST LA 6.1.2 Patch File ulilo download awali na copy file la ‘OnlineUpdateTool.exe’ na ingia kwenye location hii kwenye kompyuta yako C:\Program Files (x86)\OST LA kisha paste file hilo.

Jinsi ya Kuflash Simu Mpya za Nokia Kwa Kutumia Kompyuta

  • Bofya ‘Replace the file in the destination’ pale utakapoleta ujumbe wowote wenye kutaka ufanye hivyo.

Jinsi ya Kuflash Simu Mpya za Nokia Kwa Kutumia Kompyuta

  • Baada ya hapo hakikisha una futa au una delete file lililo andikwa ‘OnlineUpdateTool.exe.config’ hii ni muhimu sana kwani bila kufanya hivi programu hiyo itadai password ili kuweza kuitumia.

Jinsi ya Kuflash Simu Mpya za Nokia Kwa Kutumia Kompyuta

Baada ya hapo utakuwa umemaliza kuinstall programu ya kuflash simu za Nokia na sasa endelea kwenye hatua za jinsi ya kuflash simu za Nokia.

Jinsi ya Kuflash Simu Mpya za Nokia

Kwenye hatua hii na imani kuwa tayari umeshapata firmware ya simu yako kupitia link nilizokupatia hapo juu, kama bado hujapata hakikisha unadownload firmware ya simu yako ya Nokia kabla ya kuendelea kwenye hatua hizi zinazofuata.

  • Ndani ya Mafile yale uliyo install tafuta file lililo andikwa OnlineUpdateTool.exe kisha copy file hilo na paste kwenye desktop ya kompyuta yako.
  • Baada ya hapo bofya mara mbili kwenye file hilo na moja kwa moja utaona programu hiyo imefunguka.

Jinsi ya Kuflash Simu Mpya za Nokia Kwa Kutumia Kompyuta

  • Bofya Nest kisha kwenye hatua inayofuata unatakiwa kuunganisha simu yako na kompyuta, hakikisha unatumia waya maalum wa simu yako ili kuhakikisha simu yako inaunganishwa kwa urahisi na haraka.

Jinsi ya Kuflash Simu Mpya za Nokia Kwa Kutumia Kompyuta

  • Hatua hii baada ya kuunganisha simu yako unatakiwa kuzima simu yako na kusubiri ionyeshe kama ina chaji kisha weka simu yako kwenye Download Mode na unaweza kufanya hivyo kwa kubofya kitufe cha Sauti cha kupunguza pamoja na kitufe cha kuwasha, hakikisha unafanya hivyo kwa pamoja yani unabofya vitufe hivyo kwa wakati mmoja.

Jinsi ya Kuflash Simu Mpya za Nokia Kwa Kutumia Kompyuta

  • Baada ya hapo kama umefanya hatua hizi kwa usahihi utaona neno Download Mode kwenye simu yako na moja kwa moja sehemu ya ‘Edit Phone Information’ kwenye programu hiyo ya kuflash itakuwa imeonekana na kuweza kubonyezeka. Bofya hapo na subiri mpaka sehemu iliyoandikwa ‘Failed to reboot to FTM mode’ itokee kisha bofya OK kisha bofya Next.
  • Baada ya hapo hakikisha unafungua firmware ya simu yako ambayo inakuja ikiwa na file la ZIP au RAR kisha hakikisha firmware yako inakuwa na file lenye maneno haya .nb0 au .mlf mwishoni.
  • Baada ya hapo bofya sehemu yenye alama hii ya vidoti vitatu () kwenye programu ya kuflash kisha chagua file lako ambalo ulifungua awali na kisha bofya Open.

Jinsi ya Kuflash Simu Mpya za Nokia Kwa Kutumia Kompyuta

Baada ya hapo bofya Next kisha subiri kwa muda programu imalize kuflash simu yako na hakikisha unaweka simu yako mahali pazuri ambapo haito chomoka kwa bahati mbaya. Subiri imalize na baada ya hapo simu yako itajiwasha yenyewe na hapo simu yako itakuwa imamaliza kufalsh.

Mpaka hapo natumaini utakuwa umeweza kuflash simu yako ya Nokia, Hakikisha unafuata njia hizi kwa umakini na kwa usahihi kila hatua, kama kuna mahali umekwama unaweza kuuliza kupitia sehemu ya maoni hapo chini. Kama unataka kujua jinsi ya kufalsh simu za Samsung au kuflash simu za TECNO unaweza kusoma hapa.

1 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use