Kama wewe ni mmoja wa watu ambao hawapendi picha zao ziweze kuonekana kwa watu ambao huwajui basi pengine njia hii ni muhimu kwako.
Kama unatumia app ya Telegram na ungependa kujua jinsi ya kuficha profile picture yako ili watu wengine wasiweze kuiona basi makala hii ni kwaajili yako. Basi bila kuendelea kupoteza muda moja kwa moja twende kwenye makala hii.
Fungua app ya Telegram kisha bofya Menu iliyopo juu upande wa kushoto.
Baada ya hapo bofya sehemu ya Settings iliyopo chini karibia na mwisho wa menu
Baada ya hapo bofya sehemu ya Privacy and Security.
Baada ya kuchagua sehemu ya Privacy and Security, chagua sehemu ya Profile Photos.
Baada ya hapo utaweza kuona sehemu mbili kwenye Menu husika, utaona sehemu ya My Contacts na Everything. Baada ya hapo chagua sehemu ya My Contacts.
Chini ya sehemu hiyo utaweza kuona sehemu nyingine mbili, sehemu ya kwanza ni Always Allow, na sehemu ya pili ni Never Allow. Kwa kuchagua sehemu ya Always Allow itakusaidia kuweka baadhi ya magroup ya Telegram au watu ambao wataweza kuona profile picture yako.
Kwa kuchagua sehemu ya Never Allow, utaweza kuchagua baadhi ya magroup au watu ambao hutaki waone profile yako.
Baada ya kumaliza hatua zote hizo mbili moja kwa moja bofya sehemu ya tiki iliyopo juu upande wa kushoto.
Baada ya hapo utaweza kuona profile picture yako imefichwa kwa watu wote ambao umewachagua. kupitia sehemu ya pili au kama hukuchagua sehemu hiyo basi profile picture yako itafichwa kwa watu wote. Kwa kufanya hatua hizo utaweza kuficha profile picture yako
Kama unataka kujifunza zaidi unaweza kusoma hapa kujua jinsi ya kutengeneza profile picture yako ambayo ni bora zaidi kwa urahisi na haraka. Kwa maujanja zaidi hakikisha unatembelea Tanzania tech kila siku.