Kuna wakati inatokea umetumiwa picha kwenye programu ya WhatsApp na picha hizi mara nyingi inatokea zinajidownload zenyewe hivyo husababisha picha hizo kuonekana moja kwa moja kwenye Gallery ya simu yako, hii imekua ni tatizo na mara nyingi imekua ikileta kutofautiana sana baina ya watu mbalimbali sasa kama wewe umekua ukipata matatizo kama haya leo ni mwisho kwani leo tunaenda kujifunza namna ya kuficha picha na video za whatsapp zisionekane kwenye Gallery ya simu yako. Kwa kufanya hivyo itakusaidia kuwa na ulinzi wa picha zako na vile vile utakua na uwezo wa ukiziona picha zako hizo kwenye programu ya WhatsApp pekee na sio sehemu nyingine yoyote kwenye simu yako.
Kwa kuanza basi ili kuhakikisha picha zako hazionekani kwenye Gallery ya simu yako unatakiwa kuwa na simu yako ya Android au simu nyingine yoyote ile yenye uwezo wa kuwa na programu ya kuangalia mafaili yani (File Manager) na vilevile hakikisha programu ya WhatsApp ipo vizuri kwenye simu yako hiyo unayotaka kufanya zoezi hilo. Basi kama utakua umefuata hayo yote basi utakua uko nusu ya kuwezesha picha zako za whatsapp zisionekane kwenye Gallery ya simu yako.
Basi hatua ya kwanza chukua simu yako na fungua programu ya (File Manager) kama simu yako haina programu hiyo ingia (Play Store kama unatumia Android) na kisha tafuta programu hiyo kwa kuandika maneno “File Manager” tafuta programu inayo kufaa kisha (install) kwenye simu yako.
Kama umesha download programu hiyo au kama simu yako inayo programu hiyo fungua programu yako ya (File manager) tafuta folder linalo andikwa WhatsApp kisha ndani yake fungua folder lingine linalo andikwa Media ndani ya folder la media utakuta ma-folder mengine ya nane (8) yakiwemo ma-folder ya WhatsApp Media pamoja na WhatsApp Video badilisha jina la folder la WhatsApp Media kuwa (.WhatsApp Media) yani ongeza nukta mwanzo wa kila folder, pia vile vile badilisha folder la WhatsApp Video kuwa (.WhatsApp Video).
Baada ya hapo ingia kwenye Settings alafu Apps manager kisha bofya kwenye sehemu ya All alafu tafuta programu ya Gallery kisha bofya sehemu ya Clear Cache. Ukimaliza hapo moja kwa moja ingia kwenye Gallery ya simu yako hapo utaona picha zako ambazo zilikua kwenye meseji za Whatsapp hzionekani tena kwenye Gallery ya simu yako.
Hadi kufikia hapo nadhani utakua umeweza kuficha picha na video zilizoko kwenye whatsapp kutokuonekana kwenye Gallery ya simu yako, ili kujifunza haya na mengne mengi endelea kutembelea blog ya Tanzania tech au unaweza kupata habari zote za teknolojia moja kwa moja kwenye simu yako ya mkononi kwa ku-download App ya Tanzania tech kwenye simu yako ya Android, au pia unaweza kujiunga nasi kwa barua pepe pamoja na mitandao yetu ya kijamii ya Facebook, Twitter, Instagram pamoja na Yotube ili kupata habari mbalimbali za teknolojia pamoja na kujifunza mambo ya teknolojia kwa njia ya video.
Nimeipenda blog yenu kaz nzuri sana
Asante sana Edna
Nahitaji MTU kama sija msevu mamba yake kwwnye simu yangu nataka asione picha yangu iliopo kwenye profile nifanyeje?
Pongwa ingia kwenye settings za whatsapp kisha bofya privacy kisha profile photo alafu chagua My Contact. Hope imekusaidia
Maoni*mi nasema asubuh jema wa2 wakwenye whatsapp
Maoni*powavipi
Nikitaka picha zionekane tena kwenye gallery nafanyaje
Sarah kama unaswali unaweza kuuliza kwenye forum yetu, bofya kitufe cha menu kama unatumia simu kisha bofya forums kisha uliza swali lako hapo na utapata msaada wa haraka kama sekunde chache.
Simu Yangu Haikuzi Picha Za Google Nifanyeje?
John unaweza kuuliza swali lako hapa kwenye Forum yetu
Maoni*uliza ujibiwe
Niki hitaji pichaa nazionajeee nielekezeeeee manaa sizion na sijui ntaxionaj