Ni wazi kuwa smartphone ni simu binafsi kwa kila mmoja wetu, lakini kuna wakati inakuwa ni ngumu kuzuia watu wengine kutumia simu yako ndio maana leo nimekuletea njia hii ya kuficha mafile ya simu yako ya Android kwa kutumia Calculator.
Njia hii ni bora sana kwani inakusaidia kuficha vitu vya muhimu kama vile picha na vitu vingine ambavyo ungependa kuzuia watu wengine kuwaza kuona.
Hivyo basi kwa kufuata maelezo haya mafupi natumaini utaweza kukamilisha na kuficha mafaili kwa kutumia kikokotozi kwenye simu yako mkononi, lakini kumbuka kabla ya kuanza unatakiwa kuwa na simu yenye mfumo wa Android, pia hakikisha una bandle au kifurushi cha data angalau MB50 na kuendelea.
Kama unayo mahitaji hayo yote basi endelea kwa kufuata hatua hizi. Ingia kwenye soko la Play Store kisha download app inayo-itwa Calculator Vault Gallery Lock, link inapatikana hapo chini unaweza kubofya hapo na utapelekwa moja kwa moja kwenye soko la Play Store.
Baada ya kudownload app hiyo moja kwa moja sasa unaweza kufuata maelekezo kwenye video hpo chini ili kuweza kuset app hii.
Kwa kufuata maelekezo hayo moja kwa moja utakuwa umeweza kuficha mafile yako kwenye simu yako ya Android kwa kutumia Calculator.
Kwa habari zaidi za teknolojia endelea kutembelea Tanzania Tech pia unaweza kudownload App ya Tanzania Tech ili kupata habari zote za teknolojia kwa haraka, pia usisahu kujiunga na channel yetu ya Tanzania Tech ili kupata habari na maujanja mbalimbali ya teknolojia kwa njia ya video
Maoni*
jamani ahsanten kwa kutuelimisha ila naomba munisaidie namna ya kuunganisha namba ya mtu na nikapata sms zake utumiwapo na atumapo pia
sorry kwa usumbufu.
Asante kwa Kutembelea Tanzania Tech
Maoni*Mm nauliza application ya kuweza kupata taarifa hasa sms za mtu mwngne kwa kutumia simu yangu ya smartphone. maana nahc kuna mtu amenfanyia hvo
Itafaa zaidi kama mtaweka program na taratibu za Windows phone jinsi ya kuzifanyia ufumbuzi wa mambo kama ilivyo kwenye Android’s phone…
Karibu sana tunafanyia kazi swala hilo
Maoni*samhani jamani nilikuwa nauliza ni namna gani ya kuunganisha namba ya mtu kwenye simu yangu akipigiwa au akitumiwa sms na mimi inifikie
JINSI YA KUTOA PASSWORD KWENYE SIMU ZA BATANI.