Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Ficha Apps Kwenye Simu za Samsung Bila Kutumia App

Utaweza kuficha apps unazotaka bila kuinstall programu yoyote kwenye simu yako
Ficha Apps Kwenye Simu za Samsung Bila Kutumia App Ficha Apps Kwenye Simu za Samsung Bila Kutumia App
©tech-blogs.com

Ni wazi kuwa kuna wakati unahitaji kuficha app fulani kwenye simu yako, haijalishi sababu lakini ni wazi kuwa ni vizuri kuwepo kwa sehemu ambayo kwa namna moja ama nyingine itakusaidia kuficha apps kwenye simu yako.

Kuliona hili leo nimekuletea njia rahisi ambayo unaweza kutumia kufisha apps kwenye simu yako ya Android ya Samsung bila kutumia programu yoyote.

Advertisement

Njia hii ni rahisi sana na pia ni fupi hivyo hutopoteza muda mwingi wa kujaribu kufanya kwenye simu yako ya Android ya Samsung.

Jinsi ya Kuficha Apps (Samsung)

Kama nilivyo kwambia njia hii ni maalum kwa ajili ya simu za Samsung, kama unatumia simu nyingine unaweza kusoma makala hapa ya kusaidia kuficha apps.

Kwa kusema hayo moja kwa moja chukua simu yako ya Samsung, kisha moja kwa moja ingia kwenye menu ya Apps. Unaweza kuingia kwenye Menu ya apps kwa kuswipe kwa kwenda juu.

Ficha Apps Kwenye Simu za Samsung Bila Kutumia App

Baada ya kuingia kwenye uwanja wa Menu kwenye simu yako ya Samsung, moja kwa moja bofya vidoti vitatu vilivyopo upande wa kulia juu, kisha baada ya hapo chagua Settings.

Ficha Apps Kwenye Simu za Samsung Bila Kutumia App

Baada ya hapo utapelekwa kwenye uwanja wa Settings wa App drawer, moja kwa moja tafuta sehemu iliyo andikwa “Hide Apps.” Sehemu hii inapatikana mwanzo chini ya Add new apps to Home screen.

Ficha Apps Kwenye Simu za Samsung Bila Kutumia App

Baada ya kubofya sehemu hiyo, moja kwa moja utaona list ya apps zako zote ambazo ume install kwenye simu yako. Tafuta app unayota kuficha kisha ichague kwa kuweka alama ya tiki.

Ficha Apps Kwenye Simu za Samsung Bila Kutumia App

Baada ya kumaliza kuchagua apps unazotaka kuficha, moja kwa moja bofya kitufe cha back kilichopo juu upande wa kushoto.

Ficha Apps Kwenye Simu za Samsung Bila Kutumia App

Baada ya hapo moja kwa moja utaona apps hizi zimeondoka kwenye Menu kuu ya simu yako ya Samsung. Kumbuka unaweza kurudia hatua hizi ili kurudisha apps hizi zionekane.

Unatakiwa kubofya alama ya – ambayo inatokea kwenye kila apps na moja kwa moja ukisha maliza bofya alama ya back iliyopo juu upande wa kushoto ili kuweza kukamilisha hatua nzima.

Kama unataka kutumia apps hizi bila kuzirudisha kwa kutumia njia hii, unaweza kutafuta jina la app kupitia Google widget search ambapo utaweza kupata app husika na kutumia ukiwa umeificha.

Ficha Apps Kwenye Simu za Samsung Bila Kutumia App

Kama unavyoweza kuona hii ndio njia rahisi ambayo unaweza kutumia kuficha apps kwenye simu yako ya Android ya Samsung. Kama unataka kuficha apps kwenye simu yako ambayo ni tofauti na Samsung basi unaweza kusoma makala yetu hapa.

Pia kama unataka kujifunza kwa vitendo kupitia video, hakikisha unajiunga nasi kupitia channel yetu ya Tanzania Tech kwani hivi karibuni tutakuletea video bora za teknolojia zenye mafunzo bora kwa vitendo. Hakikisha una subscribe kupitia hapa ili kuhakikisha hupitwi.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use