Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Jinsi ya Kununua Bidhaa Kupitia AliExpress Ukiwa Tanzania

Ni rahisi sana mzigo kukufikia hadi ulipo hapa nchini Tanzania
Jinsi ya Kununua Bidhaa Kupitia AliExpress Ukiwa Tanzania Jinsi ya Kununua Bidhaa Kupitia AliExpress Ukiwa Tanzania

Kama wewe ni mmoja wa wasomaji wa tovuti ya Tanzania tech basi na uhakika unakumbuka ahadi niliyotoa kipindi cha nyuma ya kuelekeza njia za kukusaidia kufanya manunuzi mtandaoni. Kwa sasa tayari tumesha angalia jinsi ya kufanya manunuzi kupitia Amazon, na leo hebu tuangalie jinsi ya kufanya manunuzi kupitia mtandao wa AliExpress.

Tofauti na hatua za kufanya manunuzi kupitia Amazon, hatua za kufanya manunuzi kupitia AliExpress ni rahisi zaidi na hii inatokana na ushirikiano wa kibiashara uliopo kati ya Tanzania na China hivyo imekuwa ni rahisi zaidi kupata mzingo wako kwa urahisi bila usumbufu. Kwa kuanza labda tuangalie mahitaji ya muhimu kabla ya kuanza kufanya manunuzi ya bidhaa kupitia AliExpress.

Advertisement

Sanduku la Posta

Jinsi ya Kununua Bidhaa Kupitia AliExpress Ukiwa Tanzania

Kama wewe unategemea kufanya manunuzi mara kwa mara kupitia mtandao wa AliExpress basi nakushauri kuanza kuulizia gharama za kufungua sanduku la Posta, hii ni muhimu kwa kua mzigo wako utaenda kuchukua kwenye ofisi za posta ambazo zipo karibu na wewe au mahali ambapo ulijisalia.

Ni muhimu sana kuwa na sanduku binafsi kwani hii itakusaidia sana kuchukua mizigo yako bila usumbufu kwani ni lazima kuwa na kitambulisho ndipo utaweza kupewa mzigo wako.

Kama unahitaji kununua mzigo mara moja unaweza kutumia sanduku la posta la mtu wako wa karibu ila hakikisha mtu huyo atakuwa anapatikana kwajili ya kwenda kuchukua mzigo wako pale utakapo fika Tanzania. Kama unataka sanduku lako binafsi unaweza kujaza fomu kupitia tovuti ya posta kwaajili ya maombi ya sanduku lako binafsi, unaweza kupata fomu hiyo hapa.

M-Pesa Mastercard, Airtel Mastercard au Kadi ya Benki

Jinsi ya Kununua Bidhaa Kupitia AliExpress Ukiwa Tanzania

Hatua ya pili unahitaji kuwa na uwezo wa kununua vitu mtandaoni, kwa sasa imekuwa ni rahisi sana na unaweza kununua vitu mbalimbali kwa urahisi kupitia mitandao yako ya simu ya Vodacom Tanzania na Airtel Tanzania.

Unaweza kuchagua mtandao ambao ni bora kwako kati ya hiyo, kisha moja kwa moja jisajili na huduma ya M-Pesa Mastercard au Airtel Mastercard huduma hizi zote zinatolewa bure kabisa huna haja ya kulipia.

Kama unataka kujiunga na huduma ya M-Pesa Mastercard unaweza kusoma hapa kujua hatua kwa hatua jinsi ya kujiunga pamoja na kuweka pesa kwenye akaunti yako. Kama unatumia Airtel unaweza kuandika Menu ya Airtel Money kisha tafuta Airtel Mastercard kisha fuata maelezo.

Pakua Apps za AliExpress

Kwaajili ya kurahisisha manunuzi ni vyema kufanya manunuzi kupitia simu yako ya mkononi, hii itakusaidia kuona ofa mbalimbali za mapunguzo ya bei hivyo kama unatumia Android au iOS basi ni wakati wa kupakua App hiyo moja kwa moja kwenye simu yako.

Unaweza kubofya moja kati ya link hapo ili kupakua app hiyo moja kwa moja kupitia soko husika.

AliExpress – Android

Download App Hapa

AliExpress – iOS

Download App Hapa

Tengeneza Akaunti

Baada ya kupakua app moka kati ya hizo sasa endelea kwa kutengeneza akaunti, kwa urahisi zaidi unaweza kutumia akaunti yako ya Google kukamilisha vitu vyote kwa urahisi, kisha baada ya hapo hakikisha unaweza Tanzania kwenye sehemu ya nchi uliyopo na pia hakikisha unaweka Shipping Address kwenye ukurasa wa shipping Andress.

Hakikisha unajaza kila kitu ambacho umeulizwa na pia hakikisha unaweka Andress iliyo sasa yenye kila kitu cha msingi kama nyumba namba, namba ya simu, Jina kamili, sanduku la posta na zip code. Baada ya hapo sasa utakuwa upo tayari kufanya manunuzi ya bidhaa kupitia AliExpress.

Jinsi ya Kununua Bidhaa Kupitia AliExpress Ukiwa Tanzania

Kama utakuwa umefanikiwa kufanua kila kitu jinsi inavyotakiwa basi utaweza kuona bei za bidhaa zimebadilika na kuonekana kwa bei za Tanzania Shillings TZS. Pia hakikisha una angalia kwa chini kwenye kila bidhaa ili kuona gharama za kutuma mizigo mbalimbali kuja mahali ulipo, unaweza kuona sehemu hii kama kwenye picha hapo chini.

Jinsi ya Kununua Bidhaa Kupitia AliExpress Ukiwa Tanzania

Unaweza kuona sehemu iliyo andikwa Shipping huku kwa chini ikiwa imeandikwa njia itakayo tumiwa kufikisha bidhaa ikiwa pamoja na garama za kutuma mzigo pamoja na bei ikiwa kwenye TZS.

Hadi hapo najua utakuwa umeweza kununua bidhaa kupitia mtandao wa AliExpress, kama kuna mahali ambapo utakuwa umekwama usisite kutuandikia kupitia kwenye sehemu ya maoni hapo chini au unaweza kuanzisha mada mpya kwenye forum yetu hapa.

9 comments
  1. Kulingana na maelekezo uliyotupa hapo juu ya kutununua bidhaa kupitia alibaba (aliExpress)
    Swali
    1. Je bidhaa ikifika Tanzania nalipitia
    tena kodi au?

    2. Vipi gharama za kutoa mzigo
    kutoka dar kuja mikoani kwa hiyo
    njia ya posta mfano kutoka dar
    kuja mbeya hizo gharama nalipa
    mimi mnunuzi au ndo hiyo hiyo
    shipping fee?

    1. Mzigo haulipiwi tena lakini kuna wakati posta unayo chukulia mzigo inaweza kukulipisha kiwango fulani. Alafu ni vyema kuchagua posta iliyopo kwenye mkoa ulipo.

  2. Jina placide
    Mwanamukanda
    Mimi natamani sana kuwa mmoja kati yawanao fanya byashara kupiyia aliepress lakini nashindwa jinsi yaku make order
    Nipo south Africa

  3. Ok ningependa kujua transaction zinavofanyik hususan kwa single consumers ambao wanahitj only single product .
    Alafu nimesikia Kuna agents je Kama wapo wametapakaa tz yot I mean mikoan ambao watawez kutusaidia kupata iz hudum

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use