Jinsi ya Kufanya Kompyuta yako Kujizima kwa Wakati Maalum

Kama unataka kufanya kompyuta yako ijizime wakati fulani basi fuata video na maelekezo haya marahisi
Kompyuta Kompyuta
tesssss

Kusahau kuzima kompyuta yako kuna weza kusababisha matatizo mengi kama vile, umeme unapokuja mwingi wakati umetoka unaweza kusababisha kompyuta yako kuungua au kupiga shoti pia wakati mwingine kuacha kompyuta yako inawaka bila matumizi kwa muda mrefu kunaweza kuongeza gharama za umeme hivyo kusababisha hasara kubwa.

Ili kukusaidia katika hilo leo Tanzania tech tunakuletea namna rahisi ya kufanya kompyuta yako ijizime wakati maalum ili kukuepusha na yote hayo hapo juu, kumbuka njia hizi ni rahisi kufuata ila tu zinaitaji umakini kidogo kufuatilia hivyo usione tatizo kurudia kuangalia video au kusoma tena pale unaposhindwa kuelewa. Basi moja kwa moja twende tukaanza kuangalia hatua hizi.

Advertisement

Moja kwa moja washa kompyuta yako kisha kwenye desktop ya kompyuta yako bofya kitufe cha upande wa kulia (right click) cha mouse ya kompyuta yako kisha chagua “New shortcut“, baada ya hapo kwenye box lilopo juu ya kioo chako andika  “shutdown -s -t 600″. Kumbuka kuwa kama unataka kompyuta yako ijizime baada ya dakika 1 utaandika  t 60 hii ikiwa na maana, dakika moja inayo sekunde 60 hivyo kama unataka zaidi ya hapo utaendelea kuongeza kwa sekunde kwani hii hufanya kazi kwa sekunde pekee.

Katika mfano niliotumia hapo juu ni t 600 hivyo ni sawa na dakika 10 kwani sekunde 60 = dakika 1 hivyo 60 mara 10 = 600 ndio maana nimeandika 600 hivyo basi kompyuta yangu itajizima baada ya dakika 10. Hakikisha unaweka sekunde sahihi kisha bofya Next ili kuhifadhi shortcut hiyo kwenye kompyuta yako.

Baada ya Kufuata hatua zote hizo hapo juu, bofya mara mbili (double click) kwenye shortcut hiyo ulio tengeneza, kama unatumia Windows 7 utaona chini kwenye (Task bar) kumetokea ujumbe ambao utakua ukiashiria kuwa kompyuta yako itajizima baada ya muda maalum uliopanga hapo awali, kama unatumia Windows 10 utaona ujumbe huo katikati ya kioo chako. Baada ya Hapo utakua umefanikisha kufanya kompyuta yako kujizima kwa wakati maalum ambao umepanga mwenyewe.

Unaweza kutengeneza shortcut tofauti kwaajili ya kila saa au dakika unayota kwa mfano unaweza kutengeneza shortcut yenye lisaa na nyingine yenye dakika kumi, ili kutumia pale unapokua unataka. Kumbuka kifadhi file hilo sehemu inayo onekana ili uweze kuitumia kwa urahisi pale unapo hitaji. Njia hii ni salama kabisa na haina madhara yoyote na hufanya kazi pale tu unapo bofya mara mbili shortcut uliyo itangeneza.

Kama umependa mafunzo hayo unaweza kushare na wengine ili wajifunze pia na kama una maoni au kuna mahali umekwama usisite kutuandikia hapo chini au unaweza kujiunga na majadiliano kwenye mitandao yetu ya kijamii ya  Facebook, Twitter na Instagram pamoja na Youtube kama unataka kujifunza mambo mbalimbali ya teknolojia kwa njia ya Video. Pia kama unataka kupata habari zote za teknolojia kwa haraka unaweza kudownload sasa App yetu ya Tanzania tech kutoka Play Store na hivi karibuni itapatikana kupitia App Store.

2 comments
  1. Naomba mnifahamishe nina pc aina ya dell sasa imekuwa ikipiga shot pembeni ya kona ttzo ninini
    ila nimependa sana mafunzo yenu

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use