Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Fahamu Haya Kabla ya Kufanya Biashara Mtandaoni

Hizi hapa njia ili kufanikiwa kuanza biashara yoyote mtandaoni
Fahamu Haya Kabla ya Kufanya Biashara Mtandaoni Fahamu Haya Kabla ya Kufanya Biashara Mtandaoni

Kama wewe ni mmoja wa watu ambao wanafikiria kuanza biashara yoyote mtandaoni basi nakukaribisha kwenye makala hii, Kupitia makala hii nitakwambia mambo ambayo unatakiwa kujua kabla ya kuanza biashara hiyo ikiwa pamoja na njia za muhimu za kufuata ili kufanikiwa.

Kabla ya yote ni vyema niwa mkweli, mimi binafsi yangu bado sijafanikiwa kwa asilimia 100, ila pia siwezi kusema kuwa sijawahi kuona mafanikio ya biashara mtandaoni, hivyo nadhani kwa ujuzi wangu huo mdogo ninaweza kukupa mambo mawili matatu ambayo yamenisaidia mimi kuwa na mafanikio hayo madogo. Basi baada ya kusema hayo, moja kwa moja twende kwenye makala hii ya leo.

Advertisement

Subira ni Muhimu Sana

Fahamu Haya Kabla ya Kufanya Biashara Mtandaoni

Kama wewe ulishawahi kufanya biashara yoyote basi lazima unajua kuwa biashara yoyote inahitaji subira. Hii ni muhimu sana kuliko mambo yote kwani unaweza kuwa na furaha wakati unaanza biashara yako siku za kwanza, lakini pale unapo ona siku zinaenda na hujapata mteja yoyote basi unakata tamaa au una punguza nguvu.

Kwenye biashara mtandaoni pia unahitaji subira zaidi kuliko kitu chochote, kwani wakati unatengeneza website yako ya kwanza usitegemee kupata watumiaji wengi kwa mara moja bali jiandae kisaikolojia kuwa na moyo wa subira kwani hili huwa linachukua muda hasa kama huna pesa ya kufanya promotion.

Usipende Shortcut

Fahamu Haya Kabla ya Kufanya Biashara Mtandaoni

Kuna watu wengi sana siku hizi kufanya biashara mtandaoni ambazo hutegemea watu wengine kwa asilimia 100. Hii ni pale ambapo unakuta mtu ame tengeneza website ambayo inachukua makala au habari kutoka kwenye tovuti nyingine na mtu huyo hufanya kama vile makala hizo ni za kwake au amechapisha yeye. Mara nyingi biashara za namna hii huwa hazifanikiwi.

Kwa mujibu wa Google, biashara za mtandaoni siku hizi hutegemea zaidi brand kuliko hata makala au habari ambazo mtu anaweka kwenye tovuti yake. Hivi karibuni Google imeleta kitu kinaitwa E-A-T. Maneno hayo husimama badala ya maneno (Expertise, Authoritativeness, and Trustworthiness), hii ni njia ambayo Google hutumia kuangalia website zenye habari au makala ambazo zime andaliwa na wataalamu wa sekta hiyo.

Kwa mfano kama wewe ni dokta na unayo tovuti ya makala za afya, basi ni rahisi sana kufanikiwa kwenye biashara mtandaoni, pia vievile kama tovuti yako ipo mtandaoni siku nyingi na imejikita kwenye upande fulani maalum kwa muda mrefu basi ni rahisi biashara yako kufanikiwa. Google imetangaza kuwa kama tovuti haijatengeneza brand yake yenyewe ni ngumu kufanikiwa mtandaoni.

Fanya Biashara Inayotatua Matatizo ya Watu

Fahamu Haya Kabla ya Kufanya Biashara Mtandaoni

Kuna utofauti mdogo sana kati ya biashara bora na biashara unayopenda. Hii ni sawa na kukwambia kuwa hakikisha unafanya biashara unayopenda, lakini pia hakikisha biashara hiyo inatatua matatizo ya watu au jamii iliyo kuzunguka. Mara nyingi kama unataka kufanya biashara mtandaoni ni vizuri kuangalia changamoto ambazo wewe mwenyewe binafsi unazipata.

Hii ni sawa na kusema kuwa, wazo bora la biashara mtandaoni linatoka kwenye maisha yako ya kila siku. Kama unaona kuna uhitaji wa kuanzisha tovuti inayohusu ufugaji kwa sababu unaona ukitafuta kitu kuhusu ufugaji mtandaoni hupati kitu unacho kitaka basi go for it.. hilo litakuwa wazo bora.

Usiangalie Pesa Kwanza

Fahamu Haya Kabla ya Kufanya Biashara Mtandaoni

Point zote hizo hapo juu zinakuja kwenye point hii, Ni muhimu sana kutoweka pesa mbele kwani biashara yoyote ambayo inaweka pesa mbele huwa haina mafanikio ya muda mrefu. Nadhani wote tunakumbuka kuwa Facebook ilianza kutumika bila matangazo na ilitumika hivyo kwa muda mrefu sana zaidi ya miaka 2.

Baadae ndipo Facebook ilianza kuleta matangazo kidogo kidogo hadi sasa unaona kuwa kampuni hiyo imefanikiwa kumiliki biashara kubwa mtandao kama Instagram, WhatsApp na nyingine nyingi ambazo hazijulikani. Hapa ndio ambapo unatakiwa kujumuisha point zote hapo juu kwenye sentensi moja ambayo itasomeka hivi “kuwa na subira, usipenda shortcut na hakikisha una tatua matatizo ya watu kabla ya kuwaka pesa mbele”.

Nenda Sambamba na Mabadiliko

Fahamu Haya Kabla ya Kufanya Biashara Mtandaoni

Baada ya kufanya yote hayo hapo juu, basi hatua ya muhimu ya mwisho ni kuhakikisha unaenda sambamba na mabadiliko. Ni muhimu kujua kuwa internet inabadilika na kadri siku zinavyo kwenda mambo mengi yanazidi kupitwa na wakati na mengine yanazidi kuja kwa kasi.

Kwa mfano siku hizi unaona mtandao wa TikTok umeanza kuwa maarufu na hii inafanya Facebook na mitandao mingine kufikiria kuja na teknolojia zinazo fanana na TikTok hivyo pengine tegemea hivi karibuni kuona mengi yanayo fanana na mtandao wa TikTok kwenye mitandao mingine kama Instagram pamoja na Facebook pengine hata WhatsApp.

Ni muhimu kuendana na teknolojia pamoja na wakati kama unataka kufanya biashara yoyote mtandaoni, hivyo ni muhimu kuwa na ujuzi wa kuweza kutengeneza tovuti au biashara ambayo utaweza kuisimamia na kuendeleza hasa kwenye upande wa teknolojia.

Hitimisho

Na hayo ndio mambo ya muhimu ambayo unatakiwa kujua pale unapotaka kuanzisha biashara yoyote mtandaoni, kumbuka ni muhimu kujua kuhakikisha unafuata mambo yote haya na hapo na kuhakikishia utakuwa umepiga hatua kuelekea kwenye mafanikio ya biashara mtandaoni.

5 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use