Tume ya IEBC imesema kuwa hakuna udukuzi wowote uliofanyiwa kwenye mfumo wake wa kutoa matokeo ya uchaguzi kielektroniki, Afisa mkuu wa tume hiyo Ezra Chiloba amesema kuwa mfumo huo uko salama kabisa, imeripoti tovuti ya BBC Swahili.
Akihutubia vyombo vya habari katika makao makuu ya IEBC katika eneo la Bomas jijini Nairobi, amesema kwamba mfumo huo haukuingiliwa kabla, wakati na hata baada ya uchaguzi. Amesema kuwa maafisa wa tume hiyo waliufanyia uchunguzi mfumo huo hususan funguo zake na wakagundua kwamba hakuna tatizo lolote.
”Hakuna mtu aliyepewa funguo za kuingia katika mfumo huo hadi siku moja labla ya uchaguzi ili kuhakikisha kuwa kuna maadili’,alisema Chiloba.
Hata hivyo taarifa hizo zimekuja baada ya Bw Odinga, akiandamana na mgombea mwenza wake Kalonzo Musyoka, na viongozi wengine wakuu wa muungano huo, kusema wadukuzi walitumia taarifa alizokuwa nazo meneja wa teknolojia wa IEBC Chris Msando aliyeuawa wiki moja iliyopita kuingia katika mitambo ya IEBC na wadukuzi walitumia programu fulani kuongeza matokeo ya Rais Kenyatta na kupunguza matokeo yake, iliandika BBC.
Hata hivyo baada ya taarifa hizo Intergovernmental Authority on Development au IGAD ilitoa taarifa kuwa uchaguzi huo ulifanyika kwa uhuru na haki.
UPDATE : IEBC yajibu malalamiko ya kina Raila Odinga, Mwenyekiti wa IEBC Wafula Chebuka, andika barua – Mwananchi
Kwa habari zaidi za teknolojia endelea kutembelea Tanzania Tech pia unaweza kudownload App ya Tanzania Tech ili kupata habari zote za teknolojia kwa haraka, pia usisahu kujiunga na channel yetu ya Tanzania Tech ili kupata habari na maujanja mbalimbali ya teknolojia kwa njia ya Video.
Chanzo : BBC Swahili