Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

YouTube Yaja na Njia Mpya ya Kuzuia Mtu Kunakili Video Zako

Youtube yaleta sehemu mpya ya kuzuia watu kunakili video
YouTube video kunakiliwa YouTube video kunakiliwa

Kama wewe umekuwa mtumiaji wa mtandao wa YouTube najua utakuwa unajua tatizo kubwa lilipo la wizi wa video, hivi karibuni hata wasanii wakubwa wa muziki hapa nchini wamekuwa wakilalamika kuhusu video zao kunakiliwa na kuwekwa kwenye akaunti zingine ambazo sio zakwao.

YouTube imekuwa ikifanya mabadiliko mbalimbali kukidhi haja za watumiaji wake na sasa kuliona hili YouTube imetangaza ujio wa njia mpya ya kuzuia mtu kunakili video zako na kuzituma kwenye akaunti yake. Kupitia njia hii mtumiaji wa mtandao wa YouTube mwenye Subscriber zaidi ya 100,000 ataweza kupata sehemu hiyo ambayo endapo mtu atachukua video kutoka kwenye akaunti yako basi utapewa taarifa moja kwa moja kwa kutumia barua pepe.

Advertisement

Kupitia sehemu hiyo inayoitwa Copyright Match tool, utaweza kuchagua ni nini cha kufanya baada ya kupewa taarifa ikiwa pamoja na kuomba YouTube waondoe video hiyo iliyonakiliwa au unaweza kuwasiliana moja kwa moja na aliye chukua video hiyo.

Hata hivyo sehemu hiyo itafanya kazi endapo wewe ndio utakuwa wa kwanza kupakia (upload) video hiyo kwenye mtandao wa YouTube, na endapo labda ulipakua video hiyo kwenye mitandao mingine na mtu mwingine akaichukua na kupakia kwenye mtandao wa YouTube basi yeye ndio atakuwa mmiliki wa video hiyo kwenye mtandao wa YouTube na pale wewe utakapo pakia video hiyo aliye nakili ndio atapewa taarifa. Pia video zitakazo husika ni zile ambazo zitanakiliwa moja kwa moja yani video kamili na sio vipande vya video.

Kwa sasa sehemu hiyo itakuwa kwenye channel zenye subscribe 100,000 na kuendelea lakini kwa mujibu wa blog ya YouTube, sehemu hii itakuja baadae kwa watumiaji wote wa mtandao huo. Sehemu Mpya ya Copyright Match tool inatarajiwa kuanza kuzifikia channel hizo kuanzia wiki ijayo.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use