Ni wazi kuwa kuna wakati unataka kunakili kitu kutoka kwenye simu yako kwenda kwenye kompyuta yako bila kuchomeka waya kwenye simu yako. Hii inakuja mara nyingi kama unataka kunakili maandishi.
Sasa kama ulikuwa unajiuliza sana basi kupitia makala hii nitakupa majibu ya njia rahisi ambayo unaweza kutumia kucopy maandishi kutoka kwenye simu na kupaste moja kwa moja kwenye kompyuta yako bila kuchomeka waya kwenye simu yako.
Njia hii ni bora na inafanya kazi kwenye simu za aina zote yani android pamoja na iOS. Unacho takiwa ni kufuata maelezo hapo chini.
Kwa kuanza unatakuwa kupakua app hapo chini kupitia simu yako, changua link ya Android kama unatumia Android, au chagua iOS kama unatumia simu yenye mfumo wa iOS.
Baada ya kudownload na kuinstall app hii kwenye simu yako, hakikisha unayo akaunti ya Google kisha login kwenye app hii kwa kutumia akaunti yako ya Google. App hii hutumia akaunti yako ya Google Drive kwa ajili ya kuhifadhi mafaili kwa muda mfupi.
Baada ya hapo unatakiwa kudownload extension maalum kwa ajili ya browser yako, kwa upande wa chrome pamoja na Safari. Unaweza kutumia link hapo chini kudownload extension.
Baada ya kudownload Extension hii sasa hakikisha una login kupitia akaunti yako ile ile ya Google ambayo ulitumia kwenye simu yako. Hii ni muhimu sana.
Bofya sehemu ya Get Started kisha endelea kwa kufuata maelezo hayo moja kwa moja kwenye kompyuta yako. Kama bado huja link simu yako kwenye email hiyo basi utapewa maelezo kuwa uinstall app kwenye simu yako kwa kutumia email hiyo hiyo.
Baada ya kuinstall app kwenye simu na kwenye kompyuta moja kwa moja unaweza kutumia njia hii rahisi kwa kuangalia video hii fupi hapo chini.
Utaweza kucopy neno lolote kwenye simu na utaona notification kwenye kompyuta moja kwa moja utaweza kupaste kwa urahisi na haraka. Pia kwenye kompyuta unaweza kucopy kitu chochote na kupaste kwenye simu yako.
Bila shaka njia hii inaweza kusaidia sana kufanya mambo kwa urahisi na haraka bila kutumia waya kwenye simu kila wakati. Kumbuka unahitaji Internet kwenye simu na kompyuta yako ili kusudu njia hii iweze kufanya kazi.
Kama unataka kujifunza zaidi unaweza kusoma hapa jinsi ya kucopy maandishi kwa kutumia kamera ya simu yako.