Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Kubadilisha Word Kuwa PDF Bila Kutumia App

Utaweza kubadilisha doc au docx kuwa pdf kwa urahisi na bure kabisa bila kutumia app yoyote
Kubadilisha Word Kuwa PDF Bila Kutumia App Kubadilisha Word Kuwa PDF Bila Kutumia App

Ni wazi kuwa kama unasoma makala hii basi umekuwa mtumiaji wa mafile ya Word au DOCX na PDF kwa muda mrefu, na umekuwa ukikutana na changamoto ya kubadilisha Word kwenda kwenye PDF.

Kupitia makala hii fupi nitaenda kuonyesha njia rahisi na ya haraka ya kubadilisha Word kwenda kwenye PDF kwa urahisi na haraka bila kutumia progamu yoyote. Njia hii ni bora kwa sababu unaweza kutumia mara nyingi uwezavyo bila kulipia.

Advertisement

Basi bila kupoteza muda, moja kwa moja twende kwenye njia hizi rahisi. Kumbuka unahitaji kuwa na internet kwenye kifaa chako ili kuweza kufanya hatua hizi rahisi.

Kwa kuanza tembelea tovuti hapa chini, tovuti hii ni ya kitanzania na ina fanya kazi vizuri pengine kuliko tovuti nyingi ambazo nimewahi kutumia.

Tembelea Tovuti Hapa

Baada ya kutembelea tovuti hii moja kwa moja unacho takiwa kufanya ni kuweka file ambalo unahitaji kwenye sehemu ya choose file. Unaweza kudondoshea file kwenye sehemu ya Blue au kutumia sehemu ya Choose File kisha chagua file la Word au .Docx mahali ulipo hifadhi.

Kubadilisha Word Kuwa PDF Bila Kutumia App

Baada ya ku-upload file lako moja kwa moja utaliona kwenye chumba maalu kama inavyo onekana hapo chini. Kitu cha muhimu hakikisha unachagua file lako la Word au Docx kabla ya kubofya kitufe cha Convert.

Kubadilisha Word Kuwa PDF Bila Kutumia App

Kama unataka kuweka file zaidi ya moja, chagua sehemu yenye alama ya jumlisha juu upande wa kushoto kisha chagua mahali ulipo hifadhi file lako la Docx.

Kama kila kitu kipo sawa, moja kwa moja bofya sehemu ya “Convert to PDF” na kisha subiri kwa muda mfupi, Hakikisha ufungi ukurasa huo mpaka hatua zitakapo kamilika.

Kubadilisha Word Kuwa PDF Bila Kutumia App

Baada ya kumaliza utaona ujumbe wa kuonyesha file lako limebadilishwa kuwa PDF kikamilifu na unaweza kudownload file hilo kwa kubofya sehemu ya Download.

Kwa kufuata hatua hizi rahisi utaweza kubadilisha file lolote la Word “Docx” kuwa PDF kwa urahisi na haraka, Unaweza kurudia hatua hizi mara nyingi upendavyo hakuna gharama yoyote wala ukomo wa kutumia tovuti hiyo.

Kama unataka kujifunza zaidi unaweza kusoma hapa kujua jinsi ya kuedit PDF kwa urahisi kwa kutumia simu yako ya Android au iOS.

Kuwa wakwanza kupata habari na maujanja mbalimbali kwa kupakua app ya Tanzania Tech kupitia Play Store hapo juu.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use