Kuna baadhi ya namna mbalimbali ambazo ziko zimefichwa kwenye programu yako ya whatsapp kama ilivyo programu nyingine kama facebook messenger na nyinginezo, kwa leo tanzania tech tunaenda kukuonyesha namna ya kuandika maneno kwa staili kama vile maandishi yaliokolea maandishi yalio lala kama mcharazo na kufuta kitu ama kupigia mstari kwenye maneno.
Basi ili uanza unaitajika kuwa na toleo jipya la whatsapp kuanzia toleo la 2.12.535 na kuendelea ili kuweza kufanya trick hizi ni vyema ukawa na toleo hilo nililolitaja awali, baada ya kuhakiki kama unalo toleo jipya basi moja kwa moja fungua whatsapp yako kisha nenda kwenye jina la mtu unaetaka kuchat nae kisha anza kwa kuandika hivi.
- Ili kuandika maneno kwa kukolea yani (Bold) anza kwa kuandika *maneno yako* hapo utaona manrno yako yakiwa yamekolea.
- Kama unataka maneno yako yawe kwenye mcharazo (Italic) anza kwa kuandika -maneno yako- hapo utaona maneno yako yamekua kwenye mcharazo.
- Kama unataka kuona kuwa maneno yamekatwa (Strikethrough) anza kwa kuandika ~maneno yako~ hapo utaona maneno yako yakiwa na mkato.
Kama umeipenda hii usisite kulike page yetu ya Facebook pamoja na Twitter ili kupata habari mpya pindi zinapotoka,pia kwa kujifunza mambo mbalimbali kwa vitendo unaweza ku subscribe kwenye Youtube Channel yetu hapa.