Jinsi ya Kuondoa Root (Unroot) Simu Yoyote ya Android

Jifunze hapa hatua kwa hatua jinsi ya ku-unroot simu yoyote ya Android
Jinsi ya Kuondoa Root (Unroot) Simu Yoyote ya Android Jinsi ya Kuondoa Root (Unroot) Simu Yoyote ya Android

Ni wazi kua watu wengi sana wanatumia simu za Android ambazo zipo rooted, watu wengine hadi leo wanatafuta namna mbalimbali za kuroot simu zao. Lakini pengine leo tuangalie upande wa pili a shilingi na tuangalie njia ambazo unaweza kutumia kuondoa root (Unroot) simu yoyote ya Android.

Kwa namna yoyote unaweza kukutana na moja kati ya matatizo yafuatayo ambayo yanaweza kulazimisha kuondoa root (Unroot) kwenye simu yako ya Android. Hivyo basi yafuatayo ni baadhi ya matatizo yanayotokana na kuroot simu yako ya Android.

Advertisement

  • Kushindwa Ku-sasisha (Update) mfumo wa Android kwenye toleo jipya la Android.
  • Kushindwa kuinstall baadhi ya apps kupitia Play Store ikiwa pamoja na app ya Play Store yenyewe.
  • Simu yako kushambuliwa na malware na hivyo kustack mara kwa mara
  • Simu kuisha battery kwa haraka na kuzima bila sababu.
  • Simu kupata moto sana kuliko kawaida na kufunga programu ambazo ulikuwa unatumia.
  • Simu kushindwa kuwaka moja kwa moja na kustack kwenye logo ya kampuni ya simu.

Hiyo ni baadhi tu ya sehemu ya matatizo ambayo unaweza kukutana nayo pale unapo root simu yako ya Android, kumbuka sio lazima ukutane na matatizo yote kwa pamoja bali unaweza kukutana na tatizo moja kati ya hayo au kwenye simu nyingine unaweza usikutane kabisa na matatizo kama haya. Lakini kama umeamua kuondoa root kwenye simu yako hii ndio njia ambayo unaweza kutumia.

Kwa Kutumia SuperSU App

Kama wewe ni mtumiaji wa simu ya Android ambayo ipo rooted basi najua unajua programu ya SuperSU, app hii mara nyingi hua inahitajika pale unapomaliza kuroot simu yako. Hata hivyo programu hii pia inaweza kutumia kuondoa root kwenye simu yako ya Android, unacho takiwa kufanya ni kufuata hatua hapao chini.

  • Pakua App ya SuperSU kupitia Hapa

Jinsi ya Kuondoa Root (Unroot) Simu Yoyote ya Android

  • Baada ya kuinstall app hii ingia kwenye sehemu ya Settings ndani ya App hiyo kisha bofya sehemu iliyo andikwa Full unroot.

Jinsi ya Kuondoa Root (Unroot) Simu Yoyote ya Android

  • Baada ya hapo endelea kwenye hatua zinazofuata ambapo unatakiwa kuhakiki kwa kubofya Continue.

Jinsi ya Kuondoa Root (Unroot) Simu Yoyote ya Android

Kupitia njia hii utaweza ku-unroot simu yako ya Android kwa urahisi kabisa, kama njia hii haijafanya kazi kwenye simu yako unaweza kujaribu njia nyingine hapo chini.

Kwa Kutumia Kingo Root (Kwenye Kompyuta)

Kama wewe ulishawahi kujaribu kuroot simu yako ya Android basi lazima utakua umesha wahi kujaribu kur0ot simu yako kwa kutumia Kingo Root. Sasa mbali ya kuroot simu, programu hii pia inakuja na programu ya kompyuta ambayo unaweza kutumia kuondoa root (Unroot) kwenye simu yako ya Android. Basi kwa pamoja twende tukajaribu njia hizi kwenye simu yako.

  • Hatua ya kwanza pakua programu ya Kingo Root ya kompyuta kupitia Hapa.
  • Baada ya hapo washa sehemu ya USB Debug kwenye simu yako, kama hujui jinsi ya kuwezesha sehemu ya USB debug unaweza kuangalia video fupi hapa.
  • Baada ya hapo unganisha simu yako na kompyuta kwa kutumia kompyuta kisha utaona sehemu ikionyesha simu yako kama ipo rooted na kukutaka kuroot tena, huku sehemu nyingine ikitaka uweze kuondoa root (Unroot).

Jinsi ya Kuondoa Root (Unroot) Simu Yoyote ya Android

  • Baada ya hapo bofya sehemu ya Remove Root alafu subiri wakati simu yako ikiondolewa Root, hakikisha una subiri mpaka itakapo fika asilimia 100.

Jinsi ya Kuondoa Root (Unroot) Simu Yoyote ya Android

  • Baada ya hapo utaweza kupata ujumbe kama simu yako imeondolewa root, kumbuka njia hii ni maalum kwa watumiaji wa kompyuta za Windows hivyo kama unatumia kompyuta basi njia hii ni kwaajili yako.

Jinsi ya Kuondoa Root (Unroot) Simu Yoyote ya Android

Kwa kufuata njia hizi basi natumaini utakuwa umeweza kuondoa root (Unroot) simu yako yoyote ya Android, kumbuka kama unataka kujifunza jinsi ya kuroot simu yako unaweza kusoma hapa kama unatumia simu ya TECNO, soma hapa kama unatumia simu za Samsung.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use