Kama wewe ni mmoja wa watu wanaotumia mfumo wa Windows na ungependa sasa kuwa na mfumo mpya wa Windows 11 basi makala hii ni kwa ajili yako. Kupitia makala hii utaweza kujifunza jinsi ya ku-activate mfumo mpya wa Windows 11 kwenye kompyuta yako bila kutumia programu yoyote.
Kumbuka njia hizi zinaitaji uwe umesha install mfumo mpya wa Windows 11 kwenye kompyuta yako na kama bado hujui jinsi ya kuinstall Windows 11 kwenye kompyuta basi unaweza kusoma hapa kujua hatua kwa hatua jinsi ya kufanya hivyo.
Kama tayari umesha install mfumo wa Windows 10 kwenye kompyuta yako sasa twende nikuonyeshe namna ambavyo unaweza kuendelea kutumia mfumo huo kwa ku-activate bila kutumia programu yoyote.
Kwa kuanza unatakiwa ku-bofya hapa link hapo chini kisha copy code zote ambazo unaziona kwenye ukurasa huo.
Hakikisha unacopy kila kitu kwani ukisahau hata namba moja njia hii haitoweza kufanyakazi kwenye kompyuta yako.
Baada ya hapo tengeneza file jipya la .txt kwa kutumia kompyuta yako, mara nyingi unaweza kufanya hivi kwa kubofya sehemu ya kitufe cha kulia (right click) kwenye mouse yako kisha chagua New alafu chagua Text Document.
Baada ya hapo fungua file hilo la txt ulilo tengeneza kisha bofya kitufe cha kulia kwenye mouse yako kisha bofya paste hakikisha una paste code zote.
Baada ya hapo bofya upande wa kushoto juu kisha chagua sehemu ya Save As kisha andika jina lolote unalotaka alafu mbele ya jina hilo andika .bat hii ni muhimu sasa hakikisha jina hilo lina onekana kama hivi jinalafile.bat hakikisha mwisho kuna .bat kisha bofya Save.
Baada ya hapo utakuwa na file lenye uwezo wa kufungua au ku-activate toleo jipya Windows 10 bila kununua programu hiyo.
Bofya kwenye file hilo lenye .bat kisha bofya kitufe cha kulia kwenye kompyuta yako kisha malizia kwa kubofya Run as Administrator.
na hapo utaona ukurasa mpya umefunguka kisha baada ya hapo subiri kama nusu dakika kisha funga ukurasa huo na hapo utaweza kuona Windows 11 ime fanikiwa kuwashwa au kuwa activated.
Kumbuka kuwa makini usiharibu kompyuta yako kwani njia hizi zinahitaji ujue kompyuta angalau kidogo na kama hujui kabisa kompyuta ni vyema kuacha njia hii kabisa. Baada ya kusema hayo nadhani kama umefanikiwa kufanya hatua hizi kwa usahihi utakuwa umeweza kuwasha windows 11 yako bila kununua. Kwa maujanja zaidi hakikisha unatembelea tovuti ya Tanzania Tech kila siku.