Kampuni ya ubunifu na kutengeneza nguo ya Levis ya nchini marekani kwa kushirikiana na kampuni ya Google, mwaka 2017 kampuni hizo zilishirikiana kubuni koti janja lenye uwezo wa kufanya mambo mbalimbali kwa kushirikiana na simu janja au Smartphone.
Kwa kipindi hicho moja ya vitu ambavyo koti hilo limefanya ni pamoja kukuelekeza mtaa kwa mtaa kwa kutumia ramani ya Google Maps ambayo inasombwa kwa sauti, pia koti hilo linaweza kukupa uwezo wa kusikiliza muziki ikiwa pamoja na kusogeza muziki mbele na nyuma kwa haraka kwa kupapasa kwenye mikono ya koti hilo pamoja na mambo mengine mengi.
Siku za karibu koti hilo limeongezewa baadhi ya vitu ikiwa pamoja na uwezo wa kukupa taarifa pale unaposahau simu yako au koti hilo linapo kuwa mbali na simu. Kwa mujibu wa tovuti ya The Verge, koti hilo hutumia Sensor maalumu ambazo ziko kwenye mikono ya koti hilo ambalo hutoa mitetemeko (vibration) pamoja na mwanga maalum kwenye sehemu hizo pale tu unapokuwa umesahau kubeba simu yako au hata pale unapokuwa poteza simu yako.
Kwa mujibu wa Google ili kusudi jaketi hilo liweze kufanya kazi na kukupa taarifa za simu yako inapopotea, unatakiwa uwe umeunganisha simu yako na bluetooth ambayo pia ndio hutumika kutoa muziki kutoka kwenye simu yako na kupeleka kwenye jaketi hilo.
Koti hilo ambalo limepewa jina la Levi’s® Commuter X Jacquard tayari liko sokoni toka mwaka 2017 na unaweza kulipata koti hili likiwa na maboresho mapya ya mwaka 2018 kwa dollar za marekani $350 ambayo ni sawa na makadirio ya Shilingi za Tanzania Tsh 805,000 bila kodi na nchini Kenya unalipata kwa makadirio ya Shilingi za Kenya Ksh 36,000 bila kodi.