Kwenye historia ya teknolojia ni wazi kuwa iMac ni moja ya kompyuta zilizoleta mabadiliko makubwa ya mtazamo wa teknolojia ya kompyuta kwa miaka iliyopita. Sasa kuliona hilo, siku kama ya jana (tarehe 6 may 1998) miaka ishirini iliyopita, Steve Jobs alizindua kompyuta ya kwanza kabisa ya iMac.
Kutoka kipindi hicho hadi kufikia sasa ni wazi kuwa kompyuta za iMac zimebadilika sana, Kutoka kuwa na kompyuta zenye uwezo wa Hard Disk ya GB 4 hadi sasa kuwa na kompyuta zenye uwezo wa Hard Disk hadi ya TB 1. Kwa kipindi hicho kompyuta hiyo ya kwanza ya iMac ilikuwa inakuja na sifa za RAM ya MB 32, ukubwa wa kioo cha inch 15 pamoja na Processor yenye Speed ya MHz 233.
Kwa miaka ya sasa unaweza kuona ni kompyuta ndogo sana lakini kiukweli ukiangalia ukubwa wa hard ya kwanza iliyokuwa na uwezo wa MB 5 ambayo iliyokuwa na ukubwa kama kinanda, basi ni wazi utajua kuwa kweli hard disk ya GB 4 kwa enzi hizo ilikuwa inatosha kabisa.
Kompyuta za iMac kwa sasa ni moja kati ya kompyuta zinazotumika sana na makampuni na watu mbalimbali wanaofanya kazi kama za (Graphics,Video Design) pamoja na kazi nyingine ngumu zinazo tumia kompyuta.