Kwa kawaida kwa jinsi tunavyodhani kompyuta zipo za aina mbili tu hapa nikiwa namanisha Desktop pamoja na Laptop lakini katika ulimwengu huu mpya wa teknolojia ukisema kuwa kompyuta ziko za aina mbili watu watashangaa sana kwani sio aina mbili tena bali ni aina tatu hii ikiwa ni Laptop, Desktop na Compute Stick na hii ndio sababu hasa kwa nini unasoma posti hii.
Inawezekana labda umesha-wahi kuisikia au kuiona ila kwa faida ya wale ambao hawajawai kuiona wala kuisikia ni kwamba computer stick ni teknolojia mpya ya desktop computer ambapo unaweza kubadilisha screen ya TV yako kuwa kompyuta inayotumika moja kwa moja, ikiwa TV yako inatumia port ya HDMI basi uwezekano wa kutumia kompyuta hii ni rahisi kabisa kompyuta hii ilianza kutoka mwishoni mwa mwaka juzi ambapo ilitoka kwa awamu ya kwanza ambapo watu wengi walilamika sana kutokana na kompyuta hiyo kuwa slow sana ndipo mwanzoni mwa mwaka huu kampuni ya intel ilifanikiwa kutoa kompyuta hiyo ambayo sasa imeboreshwa zaidi.
Ikiwa na ukubwa wa GB32 Compute stick hii inauwezo wa kufanya kazi mbalimbali za kompyuta ya kawaida kama vile kuifadhi programu mbalimbali pamoja na mafaili ya muziki pia kompyuta hii inakupa uwezo wa kuongeza memory kwani ina sehemu ya memory card ambayo ina uwezo wa kutumia memory card mpaka ya GB120 vile vile kompyuta hii ina port mbili za flash ambazo zitakuwezesha kuongeza chochote kile ili kufanya matumizi yako kukamilika kabisa.
Kifaa hichi cha Compute stick kinauzwa kwa dollar za kimarekani $159 hii ni kwa nchini marekani tu inawezekana kuwa bei rahisi sana kwa sehemu nyingine dunia, kujua zaidi angalia video iliyopo hapo juu ili kuelewa zaidi kuhusu kompyuta hiyo ya Compute Stick.
Kama umeipenda habari hii unaweza kutembelea ukurasa wetu wa Facebook pamoja na Twitter pia unaweza kutembelea Youtube channel yetu ili kujifunza kwa vitendo.
Natamani kuitimu na kupewa cheti kwa njia hii.