Kwa wale wapenda game hivi karibuni Asus imezindua kompyuta yake ya kisasa ya Asus Rog gt51ca ambayo ni maalumu kwa game, kompyuta hiyo inakuja imetengenezwa kwa teknolojia ya hali ya juu sana ambapo inakuja na saa maalumu ya kuvaa mkononi ambayo inatumia (NFC) Near-Field Communication.
Kwa kutumia kifaa hicho maalumu mtumiaji wa kompyuta hiyo ya Asus Gog GT51CA anaweza kuwasha kompyuta hiyo kwa kugusa tu saa hiyo akiwa karibu na kompyuta hiyo, pia mtumiaji anaweza kuwasha sehemu maalumu ya kuhifadhi data iliyofichwa kwenye kompyuta hiyo hayo yote yanafanyika moja kwa moja kwa kutumia saa hiyo maalumu.
Kwa upande wa sifa kompyuta hiyo inauwezo wa processor ya Intel Core i7-6700K Skylake processor ambayo ina nguvu ya 4.6GHz, pia kama ungependa kuongeza memory na graphics ya kompyuta hiyo unaweza ukaongeza mpaka GeForce GTX Titan X graphics cards pamoja na RAM mpaka GB 12 kila upande. Kwa kawaida kompyuta hiyo inayo RAM ya GB 16 ya aina ya DDR4 2133MHz memory, 2800MHz pia hard disk ya M.2 PCIe 512GB SSDs.