Kampuni ya Mozilla ambayo ndio watengenezaji wa kivinjari cha Firefox, hivi karibuni imetangaza ujio wa kivinjari kipya kwa watumiaji wa simu za Android. Kivinjari hicho kinachoitwa Firefox Preview kinakuja na muonekano mpya pamoja na uwezo zaidi wa kufungua kurasa mbalimbali mtandaoni kwa haraka.
Kwa mujibu wa blog ya Mozilla, kivinjari hicho kipya kinakuja na muonekano mpya na wa kisasa zaidi huku kikirahisha matumizi pamoja na kuongezewa usalama zaidi. Mbali na hayo yote, kivinjari hicho cha Firefox Preview kina kuja na sehemu za kisasa za kuzuia matangazo kwenye tovuti unazo tembelea, pamoja na kuzuia programu za kujua ni kurasa gani ulizo tembelea pale unapo ingia kwenye tovuti fulani (Google Analytics).
Hata hivyo kupitia blog hiyo kampuni ya Mozilla ilibainisha kuwa, kupitia kisakuzi hicho kipya sehemu zote zilizokuwa kwenye kivinjari cha Firefox Focus zitaamishwa na kuamishiwa kwenye kivinjari hicho kipya hivyo kivinjari cha Firefox Focus hakitaendelea kuwekewa sehemu mpya.
Vilevile kampuni hiyo imesema kuwa kivinjari hicho kitaendelea kuwepo kwenye soko la Play Store hasi hapo itakapo tangazwa na pia kwenye muda wote huo kivinjari hicho cha zamani hakitaongezewa sehemu mpya. Kwa sasa kama unatumia Firefox Focus unashauriwa kupakua kivinjari kipya cha Firefox Preview ili kuendelea kufurahia sehemu mpya.
Kwa sasa kama unataka kujaribu ubora na muonekano mpya wa kivinjari hicho kipya unaweza kudownload Firefox Preview kupitia link hapo chini.