Suluhisho limepatikana kwa wapenzi wa mbali, hivi karibuni watafiti kutoka kwenye chuo cha City University London cha huko nchini london wamegundua kifaa na programu mpya za Android na iOS kwaajili ya kusuluhisha matatizo ya wapenzi wenye mapenzi ya mbali.
Watafiti hao kutoka london wamefanikiwa kugundua kifaa kipya cha Kissenger pamoja na programu maalum ambavyo vyote kwa pamoja vitakuwa vikifanya kazi kama lips za mpenzi wako pale mtakapo taka kuchumu (kiss) na mpenzi wako.
Kifaa hicho cha Kissenger kinafanya kazi kwa kutumia sensor maalum ambazo zinapima kiasi cha mgandamizo wa lips pamoja na sehemu mbalimbali za lips pale unapotaka kutuma busu kwa mpenzi wako wa mbali. Sehemu ya kuchumu ya kifaa hizo imetengenezwa kwa kutumia material ya silicon hivyo kuleta hisia karibia na halisi pale mpenzi wako anapotuma au unapopokea busu.
Kwa sasa watafiti hao kutoka chuo hicho cha london, wamefanikiwa kumaliza kutengeneza programu ya kifaa hicho ambayo inapatikana kwenye mfumo wa iOS, hivyo hivi karibuni jiandae kuboresha mahusiano yako zaidi kwa kumchumu mpenzi wako muda wowote akiwa mbali kwa kutumia programu na kifaa hicho kipya cha Kissenger.