Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Kioo cha Kompyuta cha Inch 24 Chenye Uwezo wa Kubebeka Mfukoni

Kama ulikua ufahamu hichi ndio kioo kipya cha kompyuta chenye uwezo wa kubebeka kwenye mkoba wako au hata mkononi
kioo-cha-kompyuta kioo-cha-kompyuta

SPUD ni kifupi cha maneno (Spontaneous Pop-up Display) hii ni aina mpya ya kioo chenye mfano wa mwamvuli chenye uwezo wa kubebeka mahali popote unapokwenda. Kioo hichi kimetengenezwa na kutolewa na mtandao wa kickstarter.com mtandao ambao ni maarufu kwa kuzindua vitu mbalimbali vya teknolojia.

Kioo hicho kipya kimetengenezwa kikiwa na sehemu za USB pamoja HDMI ambazo zitakuwezesha kuunganisha kioo hicho na simu au kompyuta yako kwa urahisi kabisa, pia kioo hichi kina uzito wa pound 2 tu sawa na kilogramu 0.907185 hivyo ni chepesi sana kubebeka mahali popote iwe mkononi au hata kwenye mkoba au begi lako. Kwa ndani Kioo hicho kimetengenezwa kwa DLP projector ambayo inauwezo wa kuonyesha resolution ya 720p (pixel), kioo hicho kinaendeshwa na battery ambayo inakaa zaidi ya masaa 6 au zaidi inategemea na matumizi.

Advertisement

Kioo hicho cha kompyuta kinategemewa kutoka mwezi june mwaka 2016 na kitakuwa kinauzwa kati ya dollar za marekani $499 sawa na shilingi za tanzania Tsh 1,100,000.

Je unaonaje kioo hichi kipya je wewe unaweza kufikiria kukinunua..? Toa maoni yako hapo chini au au unaweza kujiunga na majadiliano kwenye mitandao yetu ya kijamii ya  Facebook, Twitter na Instagram pamoja na Youtube kama unataka kujifunza mambo mbalimbali ya teknolojia kwa njia ya Video. Pia kama unataka kupata habari zote za teknolojia kwa haraka unaweza kudownload sasa App yetu ya Tanzania tech kutoka Play Store na hivi karibuni itapatikana kupitia App Store

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use