Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Kiongozi wa Samsung Alie Hukumiwa Jela Aachiwa Huru

Hatimaye mrithi wa kampuni ya Samsung aachiwa kabla ya kumaliza kifungo
Lee Jae-yong Lee Jae-yong

Kiongozi wa kampuni ya Samsung ambae pia ni mrithi wa kampuni hiyo kubwa ya kutengeneza vifaa vya kieletroniki Bw Lee Jae-yong, ameachiwa huru baada ya kuhukumiwa miaka 5 Jela.

Kiongozi huyo ameachiwa bila kutumiakia kifungo hicho chote cha miaka mitano alichopewa kutokana na makosa ya rushwa hapo mwaka jana. Hata hivyo Lee Jae-yong ambaye alihukumiwa kwenda jela mwezi wa nane (8) mwaka jana  2017 amaeachiwa huru baada ya mahakama ya rufaa ya nchini korea kusini kupunguza hukumu yake kutoka miaka mitano hadi miaka miwili na nusu, ikiwa pamoja na kutupilia mbali mashtaka ya rushwa yanayo mkabili kiongozi huyo. Kitendo kinacho mfanya kiongozi huyo kuhachiwa huru kwa sasa.

Advertisement

Hata hivyo Lee Jae-yong bado anakabili na miaka minne ya ungalizi wa polisi (Probation period) miaka ambayo Bw lee amesema tarudi kwenye mahakama hiyo ili kuhakikisha miaka hiyo nayo inafutwa.

Lee, mwenye miaka 49, pia alituhumiwa kutoa mchango wa hisani wa won 41bn ($36m; £29m) kwa nyakfu za hisani zilizosimamiwa na rafiki wa karibu wa rais aliyeondolewa madarakani Park Geun-hye. Bw Lee, ambaye pia hufahamika kama Jay Y Lee na amekuwa ndiye kiongozi wa kampuni hiyo kubwa zaidi ya kuunda simu duniani na amekuwa kizuizini tangu Februari akikabiliwa na tuhuma kadha za rushwa.

Kwa habari zaidi za teknolojia hakikisha una download App yetu mpya ya Tanzania Tech kupitia Play Store na vilevile tembelea channel yetu ya Tanzania Tech kupitia Youtube ili uweze kujifunza zaidi mambo yote ya teknolojia kwa njia ya Video.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use