Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Kiongozi Mkubwa wa Samsung Electronics Atangaza Kujiuzulu

Atangaza kujiuzulu kwa sababu alizo sema ni ‘unprecedented crisis’
Kiongozi wa Samsung Kwon Oh-Hyun Kiongozi wa Samsung Kwon Oh-Hyun
Kiongozi wa Samsung Kwon Oh-Hyun

Samsung Electronics ni moja kati ya kampuni kubwa sana za utengenezaji wa vifaa vya kielectroniki duniani, pamoja na kampuni hiyo kuongoza kwa ubora wa vifaa vyake lakini bado utawala wa kampuni hiyo unaonekana kukubwa na matatizo mbalimbali.

Hivi karibuni tulisikia kiongozi mkubwa wa kampuni hiyo Lee Jay-young, akihukumiwa miaka mitano jela kwa sababu ya kuhusiswa na utoaji wa rushwa. Lakini kama haitoshi hivi leo kiongozi mwingine mkubwa wa kampuni hiyo ametangaza rasmi kujiuzulu.

Advertisement

Kwon Oh-hyun, ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji na Makamu Mwenyekiti wa Samsung amesema kuwa amepanga kuachia ngazi ya ukurugenzi wa samsung pamoja na umakamu wenyekiti kuanzia Mwezi wa Tatu mwaka 2018.

Akieleza sababu za kujiuzulu kwenye barua aliyoituma kwa wafanyakazi wenzake Kwon amesema kuwa alikua akifikiria kwa muda mrefu sana kujiuzulu kwenye kampuni hiyo pamoja na kuwa haikuwa rahisi kufikia uamuzi huu lakini kiongozi huyo anasema sasa muda umefika kwa yeye kuachia ngazi.

Kwon aliendelea kusema kwenye barua hiyo kuwa “sasa muda umefika kwa kampuni hiyo kuongozwa na vijana ambao wataweza kukabiliana vyema na changamoto za sekta ya teknolojia inayobadilika kwa haraka kila siku”.

Aidha kwenye barua hiyo Kwon, aliongeza kuwa kujiuzulu kwake kumechangiwa na kile alicho kiita ‘unprecedented crisis’ au migogoro isyoya kawaida kwenye kampuni hiyo ambayo hakuweza kuiweka wazi, lakini kwa mujibu wa wachambuzi wa maswala ya uongozi migogoro hiyo ni pamoja na ile ya Mrithi wa kampuni hiyo Lee Jay-young kuhukumiwa kwenda jela miaka mitano.

Hii ni mara ya pili kwa mwaka huu kwa kampuni hii maarufu ya Korea kupata pigo la viongozi wakati ikiwa tayari imetoa ripoti yake ya mauzo ya kipindi cha pili cha mwaka 2017 huku ikiwa inakadiriwa kuwa mapato ya kampuni hiyo yameongezeka kwa makadirio ya asilimia 28.

Kwa habari zaidi za Teknolojia endelea kutembelea Tanzania Tech nasi tutakujuza yote mapya kwa upande wa teknolojia, pia unaweza kudownload App ya Tanzania Tech ili kupata habari zote kwa haraka zaidi.

Chanzo : Reuters

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use