Kampuni maarufu ya microsoft hivi karibuni imetambulisha kifaa kipya cha kucheza game cha Xbox one x, kifaa hicho ambacho sasa kinakuja na nguvu na uwezo zaidi wa graphics kimetangazwa hapo muda mfupi uliopita kwenye mkutano wa E3 Expo uliofanyika huko Los Angeles nchini marekani.
Kifaa hicho kipya kina sifa za 8-core CPU zenye 6 teraflops GPU pamoja na 12GB ya GDDR5 graphic memory vyote vikiwempo kwenye kava ambalo ni dogo kuliko kava la kifaa cha kwanza cha Xbox one. Kwa upande wa ukubwa wa ndani kifaa hichi cha Xbox One X kinauwezo wa TB 1 huku ikiwa na uwezo wa kusoma CD za 4K Blu-Ray pamoja na sauti iliyowezeshwa na teknolojia ya Dolby Atmos technology ambayo inawezesha spatial sound.
Xbox One X inatarajiwa kuanza kutoka kuanzia mwezi November na itauzwa kwa dollar za marekani $499 sawa na shilingi za tanzania Tsh 1,200,000. Xbox One X inatarajiwa kutoka sambamba na game 4 ambazo zitakuwa maalum kabisa kwa kifaa hicho game hizo ni
- Forza Motorsport 7
- Crackdown 3
- State of Decay 2
- Metro: Exodus
- PlayerUnknown’s Battlegrounds
- Assassin’s Creed: Origins
- Middle-Earth: Shadow Of War
Pia Kifaa hicho kitakuwa na uwezo wa kucheza game zote za kifaa cha awali cha Xbox one hivyo wataja wote pamoja na wapenzi wa game za Xbox wataweza kuendelea kufurahia game zao kwenye kifaa hicho kipya chanye maboresho makubwa na ya hali ya juu.
Kwa habari zaidi za teknolojia endelea kutembelea Tanzania Tech pia unaweza kudownload App ya Tanzania Tech ili kupata habari zote za teknolojia kwa haraka, pia usisahu kujiunga na channel yetu ya Tanzania Tech ili kupata habari na maujanja mbalimbali ya teknolojia kwa njia ya video.