Kutana na Kifaa Chenye Uwezo wa Kusikia Mawazo Yako

Utaweza kuendesha vifaa vya kieletroniki kwa kuwaza pekee
Kutana na Kifaa Chenye Uwezo wa Kusikia Mawazo Yako Kutana na Kifaa Chenye Uwezo wa Kusikia Mawazo Yako

Teknolojia inaendelea kukua kila siku na ni wazi kuwa kila siku wataalamu hufanya ugunduzi mpya unao husisha maswala ya Teknolojia na kufanya teknolojia kusonga mbele kwa kasi kubwa. Kulionyesha hili, leo nimekuandalia hii ya kifaa kipya cha kwanza chenye uwezo wa kusikia mawazo yako.

Kifaa hicho kime tengenezwa na wataalamu kutoka chuo cha MIT huko nchini marekani, na inasemekana kifaa hicho kwa sasa kinao uwezo maalum kusikia mawazo yako na kuyapeleka moja kwa moja kwenye kompyuta. Kwa maana nyingine ni kwamba, kwa sasa kifaa hicho kinasaidia mtu kufanya mambo mbalimbali kwenye kompyuta au vifaa mbalimbali ya kieletroniki kwa kutumia au kwa kusikiliza mawazo yako.

Advertisement

Jinsi kifaa hichi kinavyofanya kazi ni kuwa, kifaa hichi kina pima signal maalumu zinazohusika na mawazo ndani ya ubongo na kwenye uso wako zinazoitwa neuromuscular signals, Sasa signals hizo hutafsiri kwa kutumia mfumo wa AI au Artificial Intelligence ambao hubadilisha signal hizo kwenda kwenye mfumo wa programu ambao husaidia vitu vya kieletroniki kuweza kufanya kazi, yaani kama vile rimoti ya TV yako inavyofanya kazi lakini sasa mawazo yako ndio mkono unao bonyeza rimoti hiyo.

Kwa sasa hifaa hicho kinauwezo mdogo kama wa kusema saa pale utakapo waza ni muda gani, kutumika kuchagua programu mbalimbali kwenye TV, pamoja na mambo mengine madogo madogo. Vilevile kwa muonekano bado kifaa hicho ni kikubwa sana hivyo labda miaka ya karibuni kifaa hicho kitaboresho na hapo kutakua hakuna haja ya kutumia simu yako kumpigia mtu, bali sasa utaweza kuwaza kumpigia mtu na simu itaweza kuita hapo hapo.

Nini maoni yako kuhusu kifaa hichi..? Tuambie kwenye maoni hapo chini.

2 comments
  1. Habari mjengoni,
    Nimepakuwa happ yako haifunguki hata kidogo,
    Inaniambia error retriving network kila nitakapoifungua happ yenu

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use