Kampuni ya Nike kwa kushirikiana na kampuni ya Playstation pamoja na mchezaji maarufu wa NBA Paul George, imetangaza kuja na viatu vipya vya Nike PG-2, viatu ambavyo ni maalum kwa wapenzi wa NBA, game za PlayStation pamoja na wanaopenda kupendeza na vitu kutoka kampuni ya NIKE.
Viatu hivyo vipya vya NIKE PG-2 vime tengenezwa vikiwa na rangi pamoja na muonekano wa game ya PlayStation huku nembo za kifaa hicho pamoja na nembo ya mchezaji wa NBA, Paul George zikiwa zime tengenezwa maalum kabisa kwa ajili ya viatu hivyo.
Mbali ya nembo hizo kuwepo kwenye kiatu hicho, utofauti mwingine ni kuwa nembo hizo zina uwezo wa kuwaka mwanga wa blue sehemu inayo washwa kwa kutumia kitufe maalum kilichoko nyuma ya ulimi wa viatu hivyo.
Viatu hivyo pia vinayo namba maalum kwa nyuma ambayo itakuwezesha kupata bidhaa za PlayStation kwa punguzo kuptia maduka ya wakala wa PlayStation.
Kwa sasa bado hakuna taarifa juu ya bei ya viatu hivi lakini habari zinasema kuwa kampuni ya NIKE pamoja na Sony tayari zimesha toa tamko kuwa viatu hivyo vitapatikana dunia nzima kuanzia tarehe 10 February 2018.
Viatu hivyo ni moja kati ya viatu vya kipekee vinavyo tengenezwa na kampuni ya NIKE kwa ushirikiano na makampuni mengine, mwaka 2016 kampuni hiyo kwa kushirikiana na kampuni za teknolojia ilikuja na kiatu cha NIKE Hyperadapt 1.0 kiatu chenye uwezo wa kujifunga kamba.
Kupata taarifa lini viatu vipya vya NIKE PG-2 vitafika Tanzania, endelea kutembelea tovuti ya Tanzania Tech pia unaweza kudownload App yetu ya Tanzania Tech kupitia Play Store ili kupata habari zote mpya za teknolojia kwa haraka zaidi.