Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Kampuni ya Tigo Yatoa Kompyuta 47 Zenye Thamani ya Milioni 71

Kampuni ya Tigo inaendelea kusaidia watanzania sasa imefanya haya..
tIGO tIGO
PICHA NA NIPASHE

Kampuni ya simu za mkononi ya Tigo, imetoa msaada wa kompyuta 47 zenye thamani ya Sh. milioni 71 kwa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) ili kuimarisha juhudi za taasisi hiyo za kutoa elimu ya juu nchini, limeripoti gazeti la Nipashe

Akikabidhi kompyuta hizo, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Tigo, Simon Karikari, alisema kuwa kupitia sera ya uwajibikaji, kampuni hiyo imejikita katika kuwawezesha vijana na jamii kwa ujumla kufikia taarifa za kimataifa na uelewa na watajifunza, kupanua ubunifu wao na kushirikiana na wenzao duniani kote.

Advertisement

Alifafanua zaidi kuwa kupitia mchango huo, Tigo imeunga mkono serikali, katika mtazamo wake wa kubadilisha nchi kuwa na uchumi unaoegemea katika uelewa ifikapo mwaka 2025 na kuthibitisha kujitoa kwa kampuni hiyo katika kuunga mkono jitihada za wizara husika ya kubadilisha elimu nchini kwa kupitia kujumuishwa kwake katika uwanja wa kidijitali.

“Kupitia uwekezaji wetu wa kijamii, Tigo imekuwa mstari wa mbele katika kukuza sekta ya elimu nchini. Hatufanyi kazi tu na taasisi za elimu ya juu, bali pia tumeshatoa kompyuta na kuunganisha zaidi ya shule 60 za sekondari kwa mtandao wa intaneti wenye kasi kupitia Mradi wetu wa Shule-elektroniki.

Hali kadhalika, Tigo imetoa msaada wa madawati zaidi ya 7,100 ambayo yamewanufaisha wanafunzi wa shule za msingi zaidi ya 21,000 kote nchini “, alisema Karikari. Mgeni rasmi katika hafla hiyo, Makamu Mkuu wa Chuo cha UDOM, Prof. Idriss Kikula mbali na kuishukuru Tigo kwa mchango huo alisema.

“Ni kupitia ushirikiano huu tutaweza kutoa stadi za kisasa za Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (Tehama) pamoja na maarifa kwa kizazi cha wataalamu ili nchi iweze kukidhi mahitaji ya taarifa zinazobadilika na mtiririko wa kidijitali katika jamii na uchumi wa dunia.”

“Ninashukuru Tigo kwa utayari wake katika kushirikiana na chuo chetu ili kuongeza kiwango cha ueledi katika elimu ya kidijitali. Nakaribisha ushiriki wa wadau wengine katika utengemano wa teknolojia katika kujifunza,” alisisitiza Kikula.

Msaada huo unafuatia mkataba wa makubaliano uliosainiwa kati ya Tigo na UDOM mwanzoni mwa mwaka huu, kampuni hiyo pia imejitolea kutoa kompyuta kwa taasisi hiyo ili iweze kutoa urahisi wa kufikiwa kwa bidhaa za mtindo wa maisha ya kidijitali za kampuni hiyo.

Kwa habari zaidi za teknolojia endelea kutembelea Tanzania Tech pia unaweza kudownload App ya Tanzania Tech ili kupata habari zote za teknolojia kwa haraka, pia usisahu kujiunga na channel yetu ya Tanzania Tech ili kupata habari na maujanja mbalimbali ya teknolojia kwa njia ya Video.

Chanzo : Nipashe

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use