Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Kampuni ya Simu ya TTCL Yapewa Msamaha Deni la Bilioni 76

Deni hilo lageuzwa rasmi kuwa mtaji kwaajili ya kuboresha kampuni hiyo
TTCL Tanzania TTCL Tanzania

Kampuni ya simu ya TTCL ambayo inaongoza kwa utoaji huduma wa simu za mezani hapa nchini, hivi karibuni imepewa msamaa wa deni ililokuwa inadaiwa na serikali ya Tanzania.

Deni hilo ambalo lilikuwa linafikia shilingi za Tanzania bilioni 76 limesamehewa rasmi na waziri wa fedha na mipango wa hapa Tanzania Dr Philip Mpango. Hata hivyo waziri huyo alibainisha kuwa deni hilo sasa limebadilisha na kuwa mtaji ambapo sasa fedha hizo zitaenda kutumiaka na kampuni hiyo ya TTCL kama mtaji wa kukuza kampuni hiyo.

Advertisement

Aidha kwa mamlaka aliyonayo chini ya kifungu cha 5(3) na 9 cha Sheria ya Fedha ya Tanzania, Waziri wa fedha na mipango, Dk Philip Mpango alibadilisha deni hilo kuwa mtaji kuanzia mwezi Agosti mwaka huu.

Taarifa iliyotolewa na Msajili wa Hazina, Dk Oswald Mashindano inasema lengo la kugeuza mkopo huo kuwa mtaji ni kuitaka TTCL kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi, tija na weledi ili kuongeza ushindani katika soko.

Kwa habari zaidi za teknolojia usisahau kudownload App ya Tanzania tech kupitia Play Store nasi tutakujuza habari zote za teknolojia kwa haraka zaidi.

Chanzo : Mwananchi

2 comments
  1. Binafsi nashukuru sana kwa taarifa ninazozipata kutoka kwenu.lakini pia naomba muendelee kutupa taarifa ambazo zitaweza kutusaidia zaidi kupanuka kiteknolojia. Ahsante sana.

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use