Kampuni ya Nokia imetangaza kubadilisha alama yake (Logo) kwa mara ya kwanza katika karibu miaka 60. Alama mpya ni herufi N nyeupe kwenye duara la bluu.
Nokia imesema kuwa mabadiliko hayo yanaashiria mkakati wake wa kuzingatia ukuaji mkubwa katika soko la vifaa vya 5G.
Kwa mujibu wa Nokia, kampuni ya Nokia sasa sio kampuni ya simu pekee bali kwa sasa ni kampuni ya teknolojia kwa ujumla “business technology company”.
Hata hivyo Nokia ime bainisha kuwa, ili kuimarisha biashara yake ya vifaa vya mawasiliano, Nokia itazingatia kuuza vifaa vya kiteknolojia kwa biashara nyingine (B2B).
Hii ni pamoja na vifaa vya mtandao wa 5G na vifaa vya mawasiliano viwandani, ambavyo vitaweka kampuni ya Nokia kama washindani wa Microsoft na Amazon katika uwanja huo.
Unafikiri nini kuhusu alama mpya ya Nokia?