Miezi kadhaa iliyopita tulisikia sakata la Apple kushtakiwa na mmoja wa watengenezaji wa programu za iOS kuwa imechukua jina la Animoji bila ruhusa ya mbunifu huyo. Hatimaye kampuni ya Apple ilishinda kesi hiyo na programu ya mmbunifu huyo iliyokuwa App store toka mwaka 2014 ilitolewa.
Sasa hapo siku ya jana kampuni mmoja ya nguo ya nchini china inayoitwa Kon, imeishtaki kampuni ya Apple kwa kuiba logo yake ambayo sasa Apple wanaitumia kama nembo ya soko lake la App Store. Kwa mujibu wa tovuti ya baidu kampuni ya Kon imesaijiliwa toka mwaka 2009 na ndio ilikuwa inatumia logo hiyo.
Apple ili fanya mamboresho ya logo yake mwezi august mwaka huu 2017, kwa kuongeza rangi na kuboresha muundo wa logo yake ya soko la App Store ambapo kwa muonekano inafanana na logo ya kampuni hiyo ya china.
Kama inavyo onekana kwenye picha utofauti uliopo ni kuwa, logo ya kampuni ya Kon mistari yake iliyounda herufi A ni sawa wakati kwenye logo ya App Store imejikunja kila mwisho.
Kwa sasa kesi hiyo imepokelewa na mahakama ya nchini china na inategemewa kusikilizwa siku za karibuni. Bado mpaka makala hii inaenda hewani mahakama ya nchini humo haijaitaja kesi hiyo, endelea kutembelea Tanzania Tech kujua kitakacho jiri.
Kwa habari zaidi za teknolojia hakikisha una download App yetu mpya ya Tanzania Tech kupitia Play Store na vilevile tembelea channel yetu ya Tanzania Tech kupitia Youtube ili uweze kujifunza zaidi mambo yote ya teknolojia kwa njia ya Video.