Kwa kipindi cha hivi karibuni kampuni ya Huawei imekuwa ikikubwa na upinzani mkubwa wa kibiashara kutoka kwa marekani kupitia katazo lililo tolewa na raisi wa nchini humo la kampuni za marekani kuacha kufanya biashara na kampuni hiyo.
Kwa takribani wiki nzima, kampuni ya Huawei imekuwa ikitolewa kwenye mashirikisho mbalimbali ya kibiashara ya kampuni za marekani, kampuni ambazo Huawei hizitumia katika kutengeneza vipuri mbalimbali vinavyo tumika kwenye baadhi ya bidhaa zake.
Hata hivyo kwa kipindi chote hicho, kampuni kubwa za nchini marekani kama vile Microsoft, Intel, Google, Qualcomm na kampuni nyingine zimesitisha kufanya biashara na kampuni ya Huawei kutokana na Katazo hilo. Vilevile kampuni hiyo hivi karibuni ilipigwa marufuku kutumia memory card za Micro SD Card na SD Card kwenye vifaa vyake, kutokana na kuondolewa kwenye shirikisho la SD Association.
Sasa pamoja na yote haya ambayo unayajua na mengine huyajui, hivi karibuni huwenda taratibu kampuni ya Huawei ikawa imeanza kurudisha mambo kwenye mstari baada ya baadhi ya makampuni kuonyesha kurudisha ushirikiano na kampuni hiyo.
Kwa mujibu wa tovuti ya Android Authorty, Huawei imerudishwa kwenye shirikisho la SD Association, shirikisho ambalo ndio uhusika kwenye kudhibiti na kutoa muongozo na viwango vya utumia wa Memory card za Micro SD na SD Card kwenye vifaa vya kielektroniki. Kurudishwa huku kuna maana kuwa, vifaa vya Huawei vinaweza kuendelea kutumia memory card za Micro SD na SD Card bila katazo lolote.
Mbali na hayo, kwa mujibu wa tovuti ya 9toGoogle, hivi karibuni simu za Huawei ziliondolewa kwenye majaribio ya mfumo mpya wa Android Q, mfumo ambao kwa sasa uko kwenye hatua ya majaribio kupitia simu mbalimbali ikiwa pamoja na simu ya Huawei Mate 20 Pro. Sasa kwa mujibu wa ripoti mpya kutoka tovuti hiyo, inasemekana kuwa simu za Huawei zimerudishwa kwenye list ya simu zinazofanyiwa majaribio ya mfumo huo, na kuendelea kuungana na simu kama Tecno Spark 3 Pro na nyingine.
Kurudishwa huko kuna maana kuwa, Simu za Huawei zitapata mfumo mpya wa Android Q, mfumo ambao unatarajiwa kutolewa na Google baadae mwaka huu 2019. Hii inawezekana ni habari njema kwa watumiaji wa simu mpya za Huawei, kwani kuna uwezekano simu hizo kupata mfumo huo mpya wa Android 10 Q hata baada Huawei kupewa muda wa siku 90 kutumia mfumo kamili wa Android.
Kwa sasa, kwa mujibu wa tovuti ya CNBC, Huawei imeishtaki tena marekani, mara baada ya kampuni hiyo kuishtaki kwa mara ya kwanza marekani ikipinga sheria iliyopitisha mwaka jana inayokataza taasisi za serikali za Marekani kununua bidhaa za Huawei. Hata hivyo Mashtaka ya sasa yaliyofungiliwa na Huawei ni katika kile kinachojulikana katika masharti ya kisheria kama “mwendo wa hukumu ya muhtasari.”
Hatua hizi za kurudisha ushirikiano na baadhi ya makampuni inaonyesha huenda kampuni ya Huawei imeanza kufanya mabadiliko kadhaa ambayo pengine yanaweza kurudisha kampuni hiyo kwenye hatua yake ya kawaida. Lakini pamoja na hayo bado vikwanzo vya marekani ni vingi na huenda ikachukua muda mrefu kwa kampuni hiyo kuweza kukabiliana na vikwazo hivyo kwa wakati na kurudi kwenye hali yake ya ukuwaji kwa haraka.
Pamoja na yote bado yapo mengi ya kufuatili kuhusu sakata hili, hivyo hakikisha una endelea kutembelea tovuti ya Tanzania Tech kila siku, Kama unataka kujifunza mambo mbalimbali ya teknolojia kwa vitendo hakikisha una subscribe kwenye Channel yetu hapa.