Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Kampuni ya Google Imepanga Kuondoa Tatizo la Kutokuona Mbali

kutokuona kutokuona

Kampuni maarufu ya google imekua ikifanya kazi mbalimbali za kufanya sayansi na teknolojia kuwa msaada katika maisha yetu ya kila siku, hivi karibuni kampuni hiyo ilitangaza kuzindua huduma yake mpya ambapo kampuni hiyo itajihusisha na utengenezaji wa lensi za macho maalumu kwaajili ya kusaidia wenye tatizo la kutokuona mbali.

Hata hivyo kampuni hiyo inaamini kuwa inauwezo wa kuondoa kabisa tatizo hilo la kutokuona mbali kwa kutumia lensi hizo maalumu ambazo uingizwa kwenye macho ya mwanadamu kwa mfumo kama kimiminika na pale inapofika katika jicho hubadilika na kuwa lensi hiyo maalumu, lensi hizo huchukua nafasi ya lensi ambazo zimeharibiaka katika macho ya binadamu na kumsaidia kuweza kuona vizuri na kuondoa tatizo la kutokuona mbali bila hata ya kuvaa miwani.

Advertisement

Kifaa hicho maalumu kinaongozwa na vipande maalumu vya kompyuta ambavyo ni vidogo vidogo ambavyo hutuma  mawasiliano maalumu yaliyoko kwenye lensi hizo kwenda kwenye kifaa malumu ambacho ndio hutafsiri na kufanya lensi hiyo ibadilike shepu pale unapotaka kuona mbali. Hata hivyo mgonjwa atapaswa kutembea na kifaa hicho kila mahali anapokwenda ili kuweza kusaidia lensi hizo kutafsiri pale mgonjwa anapotaka kuona mbali, kifaa hicho kinatumia bluetooth kutuma na kupokea mawasiliano kutoka katika lensi hizo maalumu. Hata hivyo hakuna taarifa ya kwamba lensi hizo zitakua sokoni lini lakini kama kawaida ya project nyingi za Google inakubidi uwe mvumilivu kusubiria hii.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use