Kampuni ya Facebook Imenunua App Mpya ya Vijana ya “tbh”

Sasa Kujikita kwenye upande mwingine wa Vijana wa miaka 19
TBH App TBH App

Kampuni ya Facebook imenunua programu tumishi inayowalenga vijana wa chini ya miaka 19 na kuwahimiza wawe na wema wanapohusiana. App hiyo kwa jina tbh, ambayo ni ufupisho wa “to be honest” (kuwa mwaminifu/mkweli) imekuwepo kwa wiki tisa tu, lakini tayari imepakuliwa zaidi ya mara 5 milioni.

Waliounda programu hiyo wamesema inasalia kuwa programu ya kujitegemea lakini sasa watakwua na rasilimali zaidi kutoka kwa Facebook. “Tulivutiwa na njia ambazo wangeweza kusaidia kutimiza ruwaza ya tbh na kuifikisha zaidi kwa watu,” tbh wamesema.

Advertisement

Kwa mujibu wa tovuti ya TechCrunch, Facebook walinunua programu hiyo kwa “chini ya $100m”, na wafanyakazi wanne waliokuwa wanaifanyia kazi tbh sasa watakuwa waajiriwa wa Facebook. tbh wamesema ufanisi wa app hiyo unaonesha kwamba vijana wanapenda zaidi kuwa na uhusiano mwema na wa manufaa mtandaoni.

Baada ya anayetaka kutumia app hiyo kujiandikisha, huwa anaulizwa maswali mazuri na pia kupewa fursa ya kuchagua mmoja kati ya marafiki wanne. Wanaotumia hufahamishwa kwamba wamechaguliwa, lakini maelezo kuhusu nani aliwachagua hubaki siri.

tbh inaonekana kufuata mtindo uliotumiwa na Facebook nyakati za mwanzo – ilikuwa inatumiwa na kundi ndogo la wanafunzi chuoni, kisha ikawa inapatikana kwa watu wa majimbo kadha.

tbh­
Price: Free

Kwa habari zaidi za Teknolojia endelea kutembelea Tanzania Tech nasi tutakujuza yote mapya kwa upande wa teknolojia, pia unaweza kudownload App ya Tanzania Tech ili kupata habari zote kwa haraka zaidi.

Chanzo : BBC Swahili

2 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use