Kampuni ya Acer Yazindua “Swift 7” Laptop Nyembamba Kuliko Zote

Mbali na kuwa laptop nyembamba, haiuzi bei rahisi inaanzia dollar $1,699
Acer Swift 7 (SF714-51) (2) Acer Swift 7 (SF714-51) (2)

Kampuni ya Acer imekuja kivingine mwaka huu kwenye mkutano wa CES 2018, kampuni hiyo imeonyesha laptop yake ya Acer Swift 7 (SF714-51) inayo semekana kuwa laptop nyembamba kuliko laptop zote duniani.

Kwa mujibu wa kampuni hiyo, laptop hiyo ina wembamba wa 8.98mm sawa na metre 0.00898, pamoja na Acer Swift 7 kuwa nyembamba laptop hii inakuja ikiwa na processor bora ya 7th-gen pamoja na uwezo mkubwa wa internet ikiwa imetengenezewa kiunganishi cha WiFi chenye teknolojia ya 4G LTE.

Advertisement

Laptop hii inategemewa kuingia sokoni kuanzia mwezi (Aprili) wa nne ikiwa na bei ya dollar za kimarekani $1,699 sawa na shilingi za kitanzania Tsh 3,900,000. Hiyo ikiwa ni kwa mujibu wa viwango vya kubadilisha fedha vya siku ya leo, hata hivyo laptop hiyo inakuja na sifa za –

  • Uwezo wa Processor – Intel Core i7 processor
  • Ukubwa wa Hard Disk/SSD – 256GB SSD storage yenye teknolojia ya PCIe
  • Uwezo wa RAM – 8GB LPDDR3 memory
  • Uwezo wa Viunganishi – 4G LTE connectivity
  • Ukubwa wa Kioo – Kioo cha inch 14 kilicho tengenezwa kwa Corning Gorilla Glass chenye uwezo wa touchscreen ikiwa na resolution ya 1,920×1,080-pixel resolution display.
  • Uwezo wa Keyboard – Keyboard inayowaka taa au Backlit keyboard
  • Uwezo wa Battery – Inakaa Masaa 10 na chaji ikiwa imejaa
  • Mfumo wa Uendeshaji – Inatumia Windows 10
  • Ulinzi – inayo sehemu ya fingerprint reader

Kwa taarifa zaidi za mkutano wa Consumer Electronic Show (2018), unaweza kufuatilia ukurasa wetu maalum wa CES 2018 na utapata taarifa zote kuhusu mkutano huu pamoja na yote yatakayo jiri.

Kwa habari zaidi za teknolojia hakikisha una download App yetu mpya ya Tanzania Tech kupitia Play Store na vilevile tembelea channel yetu ya Tanzania Tech kupitia Youtube ili uweze kujifunza zaidi mambo yote ya teknolojia kwa njia ya Video.

1 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use